APR na Al Ahly Tripoli zatamba BK Arena
Jumapili 18.05.2025
MBB 77-87 Al Ahly Tripoli
APR 92–63 NCT
Rwanda ni mwenyeji wa shindano la BAL 2025 mkondo wa Nile Conference. Miongoni mwa timu 4 zinachuana vikali kwenye ukumbi wa BK Arena, Kigali kuanzia Jumamosi Mei 17 hadi 25 Mei 2025.
Pamoja na kwamba wachezaji wawili wa APR walipata majeraha wiki tatu zilizopita, Shema Osborn na Nobel Boungou-Colo uongozi wa APR ulichukuwa uamuzi wa kuleta wachezaji wengine wakiwemo Dylan Schommer, Sano Rutatika pamoja na mmarekani Obadiah Noel aliyekuwa akikipiga katika club ya Dar City ya Tanzania wamechukua nafasi ya Shema Osborn na Nobel Boungou-Colo waliopata majeraha makali, wakati huu wako nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Al Ahli Tripoli imepata ushindi wa pili jumapili iliibwaga Nairobi City Thunder kwa jumla ya vikapu 115-87 huku wenyeji APR BBC wakipata ushindi wa pili pia jana usiku baada kuitandika timu kutoka Afrika ya Kusini Made By Basketball kwa vikapu 103-81. Shindano hili litatamatika jumamosi tarehe 25 Juni 2025.
Shindano la BAL 2025 Mkondo wa Nile Conference Basketball Africa League, lililoanza Mei 17 linaendelea BK Arena,jijini Kigali.


Youssoupha Ndoye wa APR ni mfungaji bora, alifunga alama 25 mwenyewe
Kuhusu hali ya mchezaji mahiri Aliou Diarra ambaye alipata jeraha wakati wakichza na MBB jumapili, Kocha James Maye Jr akongea na vyombo vya habari jumapili, amesema waganga wanalifanyia kazi suala hilo na wao ndio wataamua ikiwa anaweza kuchaza jumanne hii amesema ‘’ Madaktari wa klabu wanafuatilia hali ya jeraha la mchezaji huyo raia wa Mali ambaye ametolewa nje ya uwanja katika kota ya nne ya mchezo mara baada ya kupata jeraha la la Kifundo cha mguu. Inatubidi tu tusubiri uamuzi wa daktari; sina la ziada,” Amesema Kocha James.

Kocha mkuu wa APR BBC James Maye Jr
Aidha Kocha mkuu wa APR BBC James Maye Jr, akiongea ameeleza hali halisi ya timu yake, amesema ‘’Tumejipanga vizuri tangu mwaka jana, nina kikosi kizuri licha ya kupoteza wachezaji wawili muhimu kabla ya kwenye mkondo huu wa Nile Conference kuanza lakini wamekuja wengine kuziba pengo la vijana hao’’.
Nahodha William Robeyns akiongea na Brightafrica, alikuwa na haya ya kueleza ‘’Tusahau yalitokea mwaka jana kwa timu ya APR tofaisha timu yam waka uliipita ya msimu huu, tuna wachezaji nyota (star) tulikuwa na changamoto za wachezaji waliopata majeraha leo mambo yamebadilika tuna wachezaji wenye uzoefu na benchi la ufundi safi’, ameomba mashabiki kuja kutoa hamasa tutashinda hili shindano. Nawaahidi tunakwenda Afrika ya Kusini’’.
Mwaka uliopita timu hiyo ya jeshi la Rwanda APR, ilishindwa kutinga kwenye fainali za kombe la vilabu bingwa BAL iliyofanyika Kigali mwaka jana, ilikandikwa kwenye Nile Conference 2024 nchini Senegal ikshindwa kufuzu kwenye fainali ya BAL 2024 Kigali .

Jean Jacques Boissy ni miongoni mwa wachezaji nyota wa Al Ahly Tripoli.
Leo ni mapumziko mechi zinaendelea kesho ambapo Nairobi City Thunder itapepetana na MBB Made By Basketball wakati wenyeji wakishona jasho na Al Ahli Tripoli.Timu mbili washindi katika kundi hili, wataungana na wenzao waliofuzu hivi majuzi kushiriki fainali ya Basketball Africa League BAL 2025 nchini Afrika ya Kusini mwezi ujao wa Juni.
Timu ya APR BBC ya Rwanda baada ya kufanya usajili wa wachezaji wa kigeni, inaonekana kuwa tishio katika ligi ya Afrika wakati huu ikiwa bado inaongoza ligi kuu ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini Rwanda.

Rais Paul Kagame alishuhudia mechi hiyo

Mke wa Rais Bi jeannette Kagame alishuhudia mechi hiyo pia

Uchenna Iroegbu BAL 2023 SLAC ya Guenea anakipiga katika club ya Nairobi City Thunder


Kocha mkuu wa Tripoli BBC Fouad Bou Chakra

Christopher Karenzi
