Kihara : Mchezo wa Golf kwa wachezaji wakulipwa wanapata alama kufuatia viwango vya Sunshine Development Tour.

Share Now

Na  Christopher Karenzi

Mashindano ya kimataifa ya Golf ya siku tatu yameanza rasmi jijini Kigali,yakivutia wachezaji kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika Mashariki.

David Kihara ni Mkurugenzi wa Shindano la  Sunshine Development Tour (SDT), akiongea na Brightafrica, amesema kwamba Kimsingi huu mchezo wa gofu, wanacheza kupitia kuweka mpira kwenye mashimo 18,

‘’Unahesabu ni mara ngapi umepiga mpira, yule aliyepiga mikwaju michache kabisa ndiye mshindi.  Michezo hii imepangwa kuchezwa nchini  Kenya pia,  washindi watakofuzu wataelekea Afrika ya Kusini kushiri shindano lingine la kimataifa’’.

Kihara amesema hili shindano ni la wachezaji wa Kitaaluma wanapata alama kufuatia viwango vya Sunshine Development Tour. Zawadi zitakazotolewa kwa jumla ni dola za Kimarekani  elfu ishirini na tano 25,000 USD kwa wachezaji bora 30. Aidha, bingwa wa shindano kwa kwa jumla atapewa kitita cha dolla elfu   tano 5,000 USD

Miongoni mwa wachezaji walioshiriki shindano hili ni pamoja na Nsanzuwera Celestin, mchezaji anayeendelea kung’ara na kwa sasa anaongoza wachezaji wa Kanda ya Afrika Mashariki. Nsanzuwera, ambaye amekuwa mchezaji wa kulipwa kwa zaidi ya miaka mitano, amesema kuishi karibu na uwanja wa kimataifa wa Golf kumempa hamasa kubwa, kumsaidia kujiandaa ipasavyo na pia kumpa nafasi ya kukutana na wachezaji wa kulipwa (professionnels), hali iliyomsaidia kupiga hatua katika mchezo huu.

Akizungumza na waandishi wa habariNsanzuwera amesema kuwa Wanyarwanda waliomo kwenye mashindano haya wako tayari kushinda na kwa kuwa wanacheza nyumbani, wanapaswa kuonyesha kiwango bora zaidi.

Kuhusu matarajio yake ya baadaye, Nsanzuwera ambaye anaongoza nafasi ya kwanza Afrika Mashariki, alieleza kuwa mashindano haya ni maandalizi muhimu kuelekea mashindano ya kimataifa yatakayofanyika Afrika Kusini. “Bado niko kwenye kiwango ninachojifua nacho, nitaendelea kujituma ili nisipoteze nafasi. Wiki ijayo tunayo mashindano mengine nchini Uganda, hivyo ni kuendelea na mazoezi na kujiandaa kupitia mashindano haya,” amesema.

Mashindano ya Kigali yanatangulia mkutano mkubwa wa SportsBiz Africa,unaolenga kuunganisha michezo na biashara.Nsanzuwera amebainisha kuwa moja ya njia kuu za wachezaji kujiendeleza ni kupitia udhamini na matangazo ya kampuni, ndani na nje ya nchi, yanayowawezesha kushiriki mashindano ya kimataifa bila gharama kubwa binafsi.

Habari hii inaonyesha wazi jinsi Golf inavyozidi kukua Rwanda na nafasi ya wachezaji wa ndani kushindana kimataifa.

Njorogi Kibugo ni mchezaji  kutoka nchini Kenya amesema kwake ilikuwa siku ngumu lakini kesho bado ana kibaruwa katika shindano hili la Gofu anataraji kujikakamua na kufanya vizuri.

 “Ni mchezo wa mashabiki na pia barani Afrika kuna fursa nyingi. Hakika kuna njia ya kusonga mbele, kuna mustakabali, na naamini watoto watapata taaluma kupitia mchezo huu.” Amesema Kibugo.

Mashindano haya ni kituo cha tano cha msimu wa Sunshine Development Tour – East Africa Swing 2025, yakileta pamoja zaidi ya wachezaji 120 wa gofu kutoka nchi 16. Shindano hili la gofu litatamatika  ijumaa tarehe 5 Agosti 2025


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *