Trump na Harris waafikiana kushiriki mdahalo wa televisheni Septemba 10.

Share Now

Mgombea urais wa cahama cha Republican na rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema kuwa wamekubalina na mgombea urais wa chama cha Democrat Kamala Harris kuwa watafanya mdahalo wa televisheni Septemba 10 mjini Philadelphia

Donald Trump ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth kwamba wapinzani hao wamekubaliana kuwa mdahalo huo kwenye kituo cha televisheni cha ABC News utaendeshwa chini ya sheria sawa na mdahalo wa kituo cha CNN uliofanyika mnamo Juni 27, bila kuwepo watu jukwaani na kipaza sauti cha kila mgombea kuzimwa wakati mwenzake anapozungumza.

Lakini makamu wa rais Kamala Harris hajabainisha kuwa wameafikiana na mpizani wake kushiriki mdahalo huo.

Wakati huo huo, makamu wa rais Kamala Harris na gavana wa Minnesota Tim Walz, wamekubali kufanya mahojiano yao ya kwanza ya pamoja.

Awali Licha ya Trump alikishtumu kituo cha televisheni cha ABC News kwa kuwa na upendeleo.

Wanasiasa hao watafanyiwa mahojiano na kituo cha televisheni cha CNN katika jimbo la Georgia siku ya Alhamisi.

Mahojiano hayo na kituo cha televisheni cha CNN yanatokea baada ya hotuba walizozitoa wakati wa kongamano la kitaifa la chama cha Democrat lililofanyika mjini Chicago- hafla iliyoandaliwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Mahojiano hayo yatakuwa ya kwanza ya kina na chombo cha habari tangu Rais Joe Biden alipojiondoa kwenye kinyang’anyiro cha urais zaidi ya wiki tano zilizopita na kumuidhinisha Kamala Harris kama mbadala wake.


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *