Mkopo wa Milioni zaidi ya Milioni 26 Dola za Kimarekani kati ya Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo na serikali ya Rwanda
Na Christopher Karenzi
Rwanda yaaendelea na mpango wa kuboresha usafiri wa umma, likiwa na lengo kwamba mabasi ya usafiri wa abiria yatapaswa kutumia nishati ya umeme. Katika juhudi za kukabiliana na uchafuzi wa hewa unaosababishwa na uzalishaji wa gesi chafu, mabasi yameongezwa katika barabara za Kigali mwaka huu 2016.
Kuna mpango wa kutengeneza Stendi kubwa ya mabasi, Iliyopo sasa hivi Nyabugogo haitosherezi kwa mabasi yanayokwenda mikoani na nchi za nje kama abiria wanavoelezea changamoto zilizopo.

Faida ya mabasi haya ya umeme ni kwamba yana mwendo kasi sana na hayakosi abiria mara kwa mara.
Kituo cha mabasi kinahitaji kupanuliwa. Mimi hupenda kusafiri mara kwa mara, na wakati mwingine ninapotembelea vituo vingine vya mabasi, naona kuna tofauti ikilinganishwa na Nyabugogo; huko kunaonekana kuwa na msongamano na ukosefu wa mpangilio.
Kituo hiki cha mabasi kikiboreshwa, msongamano wa magari utapungua. Kuna magari yanayotoka mikoani yakishusha abiria huku mengine yakiwa yanasubiri kupakia abiria, ilhali kituo cha mabasi ni kidogo.
Makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali ya Rwanda na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo, walikubaliana mkopo wa dola za Kimarekani milioni 26 na Laki mbili.
Waziri wa nchi katika Wizara ya Fedha na Mipango Godfrey Kabera, amesema kuwamkopo huo utasaidia kuboresha usafiri wa umma, ikiwemo ukarabati na uboreshaji wa Kituo cha Mabasi cha Nyabugogo,jinni Kigali pamoja na kuongeza idadi ya mabasi yanayotumia umeme.
Kwa ujumla, mpango wa kitaifa wa kutekeleza matumizi ya magari rafiki kwa mazingira yanayotumia umeme, unaendelea kupanuliwa na kuimarishwa.
