‘’Visit Rwanda’’ Final  ya ushindi mkubwa  kwa Rwanda

Share Now

Christopher Karenzi

Hata kabla ya kipenga cha kuanza kwa fainali ya UEFA Champions League inayochezwa katika uwanja wa Puskás Aréna mjini Budapest, Hungary,  tarehe  30 Mei 2026, saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, kati ya Paris Saint-Germain (PSG) na Arsenal, sehemu kubwa ya watazamaji wanaokadiriwa kufikia kati ya milioni 450 hadi 500 duniani, tayari walikuwa wanamfahamu  au walikuwa wamegundua  mshindi ambaye hayupo uwanjani.

Mshindi huyo ni Rwanda, taifa dogo lakini lenye maono makubwa kutoka Afrika Mashariki, ni  mshirika wa vilabu vyote viwili vilivyofika fainali kupitia kampeni yake maarufu ya utalii ya “Visit Rwanda”.

Kwa miaka kadhaa sasa, kaulimbiu ya “Visit Rwanda” imekuwa ikionekana wazi kwenye mikono ya jezi za Arsenal na katika mazingira ya kibiashara ya PSG.

Huu ni ushindi mkubwa wa diplomasia ya michezo, utalii na utangazaji wa taifa katika jukwaa la kimataifa.

Kwa mtazamo wangu, hii ni moja ya fainali ngumu sana kutabiri kati ya Paris Saint-Germain na Arsenal. PSG wana uzoefu mkubwa wa mechi kubwa na wana safu kali ya ushambuliaji, lakini Arsenal ya Arteta imekuwa timu yenye nidhamu, presha kubwa na ulinzi imara sana msimu huu.

Kuhusu “Visit Rwanda”, hii final ni ushindi mkubwa sana kwa Rwanda bila kujali nani anachukua kombe. Sababu kubwa ni kwamba klabu zote mbili zina uhusiano na kampeni ya Visit Rwanda:

Hivyo duniani kote watu wataona brand ya Rwanda kwenye moja ya matukio makubwa zaidi ya michezo duniani. Watu wengi sasa wanaanza kuhusisha Rwanda na football kubwa, Utalii na Kuwekeza kupitia  ushirikiano huu.

Kwa upande wa branding na sports diplomacy, Rwanda tayari imeshinda hii finali

Kwa upande wa branding, Rwanda imepata value kubwa sana kuliko nchi nyingi za Afrika zinazowekeza kwenye matangazo ya kawaida

Arsenal ni mshirika wa udhamini wa nembo kwenye mkono wa jezi.
(Yaani nembo ya “Visit Rwanda” huonekana kwenye sehemu ya mkono wa jezi za Arsenal.)

PSG ni mshirika mkuu wa kibiashara na kimatangazo.
(Hii ina maana “Visit Rwanda” ina ushirikiano mpana zaidi wa matangazo, biashara na utambulisho wa kimataifa ndani ya shughuli za PSG.)

Tusubiri hadi kipenga cha mwisho kupulizwa ndipo dunia itakapofahamu iwapo ni Arsenal au Paris Saint-Germain watakaotwaa taji la UEFA Champions League mwaka 2026.

Lakini jambo lililo wazi tayari ni kwamba fainali hii imeandika historia kubwa, si kwa vilabu pekee bali pia kwa Rwanda kupitia kampeni yake ya “Visit Rwanda”, ambayo imeendelea kung’ara katika jukwaa la soka la kimataifa


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *