Charles Gacheru: Kupokea shindano kama hili si uwanja pekee tu bali hata miundombinu na mazingira salama

Share Now

Na Christopher Karenzi

Shindano la kimataifa ya Golf SportsBiz Africa Championship  linafikia kilele chake mjini Kigali Ijumaa, Septemba 5, 2025.
Mkenya Charles Gacheru, ambaye ndiye msimamizi wa shughuli na masoko ya mashindano ya Golf yajulikanayo kama Sunshine Development Tour – East Africa Swing, amesema kwamba uamuzi wa kuyapeleka Rwanda ulifanywa kwa kuzingatia zaidi ya uwanja pekee.

Kuhusua suala la michezo na biashara (Golf SportsBiz Africa) linavoingiliana kwenye michezo  amesema kuwa miundombinu ya Kigali, urahisi wa usafiri, hoteli za viwango cya juu na mazingira salama, vyote vilihesabika kama sababu kuu ya kushiriki mashindano hayo ya kusissimua.

Kukubali mashindano kama haya hakuishii kwenye uwanja mzuri pekee, bali kunaangaliwa pia mambo mengine kama hoteli, usafiri wa wachezaji na walezi wao, pamoja na mambo mengine. Rwanda imethibitisha uwezo wake wa kupokea michezo na mikutano ya kimataifa kwa kiwango cha juu,” alisema Gacheru.

Akitolea mfano, alikumbusha kwamba Rwanda imewahi kufanikisha kwa ubora mikutano na matukio kama vile Kongamano la FIFA, Mkutano Mkuu wa FIA, Basketball Africa League (BAL)na Tour du Rwanda.

Kuhusu uwanja wa mashindano, Gacheru alisisitiza kwamba Kigali Golf Resort & Villas ni moja ya viwanja bora kabisa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, na kimekidhi vigezo vyote vya mashindano makubwa ya kimataifa ya Golf.

“Ni miongoni mwa viwanja vya juu tulivyonavyo katika eneo hili, na kwa kweli naweza kusema ni bora zaidi Afrika Mashariki na Kati. Ndicho kigezo kingine kilichotufanya tulete mashindano haya Kigali,” aliongeza.

Kwa ujumla, Gacheru alisisitiza kwamba mchanganyiko wa miundombinu, urahisi wa usafiri, hoteli na uwanja wa kisasa wa Golf, ndio uliofanya Rwanda kuwa mwenyeji wa toleo la tano la Sunshine Development Tour – East Africa Swing.

Shindano ya SportsBiz Africa Golf Championship yamedhaminiwa  na SportsBiz Africa, Kenya Breweries Limited kupitia chapa chake cha Johnnie Walker, Kigali Golf Resort & Villas, na Pure Travel.

Mkenya Charles Gacheru,msimamizi wa shughuli na masoko ya mashindano ya Golf


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *