Mashindano ya Gofu ya SportsBiz Africa yatua Kigali – Septemba 3–5, 2025
Na Christopher Karenzi
SportsBiz Africa, kwa ushirikiano na Sunshine Development Tour – East Africa Swing, wameandaa mashindano makubwa ya gofu barani Afrika yatakayofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Septemba 2025 katika viwanja maridadi vya Kigali Golf Resort & Villas, nchini Rwanda.
Mashindano haya ni kituo cha tano cha msimu wa Sunshine Development Tour – East Africa Swing 2025, yakileta pamoja zaidi ya wachezaji 120 wa gofu kutoka nchi 16. Kati yao ni Haydn Porteous kutoka Afrika Kusini, bingwa mara mbili wa DP World Tour, ambaye ataongoza kundi la wachezaji nyota kutoka Afrika, Ulaya, na Amerika Kaskazini. Kwa mujibu wa ngazi husika zawadi kwa mshindi ni kitita cha USD 25,000 (sawa na RWF milioni 36.2)
Muundo: Mashindano hayo ya siku 3 (mashimo 54), na mchujo baada ya mashimo 36 (wachezaji 30 bora na waliotoka sare wataendelea). Alama: Zinahesabiwa kwa Sunshine Development Tour Order of Merit, OWGR (viwango vya dunia), na WAGR (wachezaji wa ridhaa)
Wachezaji Mashuhuri wanaotarajiwa kushiriki ni pamoja na Haydn Porteous (Afrika Kusini) Bingwa mara 2 wa DP World Tour, Celestin Nsanzuwera (Rwanda) Bingwa wa Johnnie Walker Classic, Diani, Njoroge Kibugu (Kenya), Bingwa mara 2 wa SunDev Tour msimu huu
Aidha, upande wa Wachezaji nyota wanawake watakaoshiriki ni pamoja na Ivanna Samu (Afrika Kusini), Naomi Wafula (Kenya), Irene Nakalembe (Uganda) na Noeline Narubega kutoka (Rwanda) Mwanariadha chipukizi anayeng’ara.

