EAPCO 2023:Askari Polisi wa Rwanda watwaa vikombe 9
Rwanda imekuwa mwenyeji wa mashindano ya askari polisi kutoka mataifa ya ukanda wa Afrika ya mashariki ‘Eastern Africa Police Chiefs Cooperation Organization (EAPCCO)’. Mashindano haya yalianza tarehe 21-27 Machi 2023 mjini Kigali.
Mashindano hayo yameandaliwa chini ya kaulimbiu ‘’ Kukuza ushirikiano wa polisi katika kupambana na uhalifu unaovuka mipaka pamoja na ushirikiano wa polisi kupitia michezo na burudani’’.

Kamanda mkuu wa Askari Polisi Rwanda “IGP”, DCG Namuhoranye Felix akikabidhi kombe mchezaji
Michezo ya EAPCO 2023 imezileta kwa pamoja Uganda,Kenya, Sudani Kusini, Burundi, Ethiopia, Kenya, Sudani na mwenyeji Rwanda ambayo imepokea kwa mara ya kwanza Awamu ya nne ya mashaindano hayo.
“EAPCCO Games 2023”, Timu ya Polisi ya Rwanda imemaliza ikiwa kwenye nafasi a kwanza baada ya kunyakua vikombe 9 kati ya michezo 13 iliyochezwa.

Timu zilizoshiriki michezo mbali mbali ikiwemo soka, Volleyball, riadha, Basketball, Darts, Ndondi, Basketball, Handball, Judo, Karate, Taekwondo, Netball, na kulenga shabaha “Shooting’’. Wachezaji wote kwa jumla walioshiriki walikuwa 1250 wanaume na wanawake.
Katika mchezo wa soka, timu y Askari Police ya Rwanda ilifunga ya Burundi kwa mikwaju ya penati baada ya timu hizo kuondoka suluhu kwa magoli 3-3. Mechi ya kwanza Police ya Rwanda iliinyuka Burundi maarufu Rukinzo kwa magoli 3-1 na mechi ya pili Timu ya Polisi Burundi ikaibwaga Rwanda 2-0. Baada ya dakika 120 timu zote zikiwa sare ya 3-3 ilipigwa mikwaju ya penati Rwanda ikaingiza 5-4 Police ya Burundi, kombe likabaki nyumbani Rwanda.

Kwa jumla Askari Polisi wa Rwanda, walinyaka nafasi ya kwanza, Kenya ni ya pili wakati Uganda ikija kwenye nafasi ya 3.
Timu askari Polisi ya Uganda ilinyakua kombe la Netball iyochezwa na wanawake, Tanzania ilitwaa kombe la Darts wanaume, Kenya ilitwaa kobe la riadha wakati Burundi ilitawazwa kombe la Judo.
Rwanda ilizolea vikombe vya Basketball, Volleyball, Ndondi, Karate, Kulenga shabaha kwa kutumia bunduki na Pisto, waliibuka pia kombe la soka, Handball.


Christopher Karenzi
