Wachezaji 23 wa timu ya Amavubi waitwa  kwa Michezo dhidi ya Benin na Afrika Kusini

Share Now

Na Christopher Karenzi

chriskarenzi@gmail.com

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Rwanda Amavubi, Adel Amrouche, ametangaza orodha ya wachezaji 23 atakaotegemea katika harakati za kufuzu Kombe la Dunia la mwaka 2026, kwenye michezo Rwanda itacheza na Benin pamoja na Afrika Kusini mwezi huu.

Jioni ya Jumatano, tarehe 1 Oktoba 2025, Kocha Amrouche alitangaza hadharani majina ya wachezaji aliochagua kwa michezo hiyo miwili.

Miongoni mwa wachezaji waliitwa kwa mara ya kwanza ni mshambuliaji Joy-Lance Mickets, mwenye umri wa miaka 31, anayechezea Sabah FK katika Ligi Kuu ya Azerbaijan, ambaye tayari amefunga mabao matatu katika msimu wa 2025/26.

Mshambuliaji Joy-Lance Mickets

Wachezaji hawa watacheza dhidi ya Benin tarehe 10 Oktoba kwenye Uwanja wa Amahoro, kabla ya kukamilisha ratiba kwa kumenyana na Afrika Kusini tarehe 14 Oktoba 2025.

Orodha ya Wachezaji:

Walindamlango

  • Ntwari Fiacre
  • Buhake Twizere Clement
  • Ishimwe Pierre

Walinzi (Makipa)

  • Mutsinzi Ange
  • Manzi Thierry
  • Kavita Phanuel
  • Mbaya Byiringiro Jean Gilbert
  • Niyomugabo Claude
  • Nkurikiyimana Daryl Nganji
  • Nshimiyimana Emmanuel
  • Nshimiyimana Yunusu

Viungo:

  • Bizimana Djihad
  • Mugisha Bonheur
  • Muhire Kevin
  • Ruboneka Jean Bosco
  • Hamon-Aly-Enzo
  • Ishimwe Annicet

Washambuliaji:

  • Mugisha Gilbert
  • Kwizera Jojea
  • Nshuti Innocent
  • Biramahire Abbedy
  • Gitego Arthur
  • Joy-Lance Mickets

Hali ya Kundi C:

Kwa sasa, kundi C linaongozwa na Benin yenye alama 14, sawa na Afrika Kusini iliyo nafasi ya pili. Nigeria ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 11, sawa na Rwanda iliyoko nafasi ya nne. Lesotho ipo kwenye nafasi ya tano ikiwa na pointi 9, huku Zimbabwe ikiwa ya mwisho kwa pointi 4 baada ya michezo 8.

Inatarajiwa kuwa wachezaji wote waliotajwa wataanza kambi rasmi Jumatatu, tarehe 6 Oktoba 2025


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *