TotalEnergies yashtumiwa kwa uhalifu nchini Msumbiji

Share Now

Kituo cha Ulaya cha Haki za Kikatiba na Kibinadamu (ECCHR) kimewasilisha malalamiko ya kisheria dhidi ya kampuni ya TotalEnergies, na kuishtumu kwa kuhusika katika uhalifu wa kivita katika eneo lake la gesi Msumbiji.

Kulingana na DW, Waraka ulioonekana na shirika la habari la AFP, umesema malalamishi hayo yaliwasilishwa na shirika hilo lisilo la kiserikali la Ujerumani jana na mwendesha mashtaka wa kitaifa wa Ufaransa dhidi ya ugaidi.

Waraka huo unaangazia madai ya unyanyasaji kati ya Julai na Septemba 2021 uliofanywa na wanajeshi wa kikosi kazi cha pamoja (JTF) kilichotumwa kulinda eneo hilo la gesi  Msumbiji ambalo kampuni hiyo inasimamia na kupanga kuanzisha tena baada ya shambulizi la itikadi kali.

ECCHR imesema nyaraka za ndani zinaonyesha kuwa TotalEnergies ilifahamu kuhusu tuhuma za unyanyasaji dhidi ya raia zilizofanywa na wanajeshi hao lakini iliendelea kuwaunga mkono.

Kulingana na ECCHR, kampuni hiyo imekanusha kufahamu kuhusu madai hayo ya unyanyasaji.

Nembo ya kampuni ya mafuta ya TotalEnergies

Brightafrica.rw


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *