Mkuu wa Sekta ya Fedha Asiimwe : EADB ni mshirika imara wa maendeleo kwa Rwanda

Share Now

Na Christopher Karenzi

chriskarenzi@gmail.com

Jijini Kigali Jumanne tarehe 16 Desemba 2025,  kumefayika mkutano wa siku moja ambao umeandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika ya Mashariki ( EADB). Mkutano huu umeandaliwa chini ya kaulimbiu isemayo: Mchango wa Ufadhili wa EADB katika Mageuzi ya Kijamii na Kiuchumi ya Rwanda.” Lengo ni kuangazia mchango wa Benki katika maendeleo ya Rwanda kupitia ufadhili jumuishi na wa kimkakati.

East Africa Development Bank (EADB) ina mpango wa kutoa mikopo kwa jumla ya Milioni 150 of US $ kwa miradi mbalimbali mwaka ujao wa 2026

Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha nchini Rwanda, Bw. Herbert Asiimwe,

Akizungumza katika kikao cha wadau kilichoandaliwa na Benki hiyo,  Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha nchini Rwanda, Bw. Herbert Asiimwe, aliyemwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango ya Kiuchumi (MINICOFIN) nchini Rwanda,  amesema kuwa EADB imekuwa mshirika imara wa maendeleo kwa Rwanda kwa miaka kadhaa.

“Programu za ufadhili za EADB zimeimarisha sekta muhimu za uzalishaji kama vile viwanda, kilimo, usafirishaji, mali isiyohamishika, biashara, makazi na sekta ya SME, hivyo kuchochea shughuli za kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi kote Rwanda,” Amesema Bw. Asiimwe. Amebaini kuwa, “Uwekezaji wa EADB umechangia moja kwa moja katika malengo ya kipaumbele ya Maendeleo Endelevu ya Rwanda kwa kuunga mkono shughuli za kuzalisha kipato na kuleta matokeo yanayolingana kikamilifu na Dira ya Rwanda 2050, inayolenga ukuaji shirikishi, endelevu na unaoongozwa na sekta.”

Kwa historia fupi, Benki hiyo ilianza mwaka 1967 na wanachama wa Jumuiya ya mwanzo  ya Afrika ya Mashariki  kabla haijavunjika. Benki iliendelea kuwepo pamoja na kwamba  Jumuiya ilikuwa imevunjika, Kwa mujibu wa Bwana Benard, Jumuiya  ilipoanzishwa upya Benko imeendelea kuwepo na Makao makuu yako jijini Kampala,  Uganda.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ya Mashariki   EADB , Bw. Benard

Jukumu la benki hiyo ni nini hasa?

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ya Mashariki  ( EADB) , Bw. Benard amesema : ‘’Jukumu lake  kuu ni kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Afrika ya Mashariki na EADB ni  mojawapo ya taasisi  ambazo zinaorodheshwa  kama Taasii za Jumuiya’’ .

Mwaka 2008, Rwanda ilijiunga rasmi kama mwanachama, mwanahisa wa Benki ya Maendeleo ya ya Afrika ya Mashariki.

Kwa wakati huu sasa kuna wanahisa wanne ikiwa ni pamoja na Serikali za Tanzania,Kenya Uganda na Rwanda. Kwa mujibu wa Bwana Benard, kuna mpango wa kwenda nchini Burundi kuongea na nchi jirani ya Burundi ili kwa miaka ijayo waanzishe Benki hiyo ya Maendeleo. Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) imetoa kwa jumla dola za Marekani milioni 33 (sawa na takribani faranga za Rwanda bilioni 48) kwa taasisi nne washirika nchini Rwanda tangu kuzinduliwa kwa Mpango wake wa SME wa mwaka 2024.

Bi Kaberuka (kushoto) ni miongoni mwa akina mama walionufaika kupata mkopo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ya Mashariki  (EADB)

Fedha hizo zimepitishwa kupitia taasisi za kifedha washirika ambazo ni Benki ya Maendeleo ya Rwanda (BRD), Duterimbere IMF Plc, AB Rwanda Plc na Letshego Rwanda. Ufadhili huo umeziwezesha biashara ndogo na za kati (SME) katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, viwanda, biashara, makazi na usafirishaji.Hatua hiyo imefikia hatua ya kubuni  zaidi ya ajira 7,000, zikiwemo ajira za kudumu zaidi ya 4,000 na ajira za muda zaidi ya 3,000. Asilimia 40 ya ajira hizo zimewanufaisha wanawake.

Malipo hayo ni sehemu ya Mfuko wa SME wa EADB wa thamani ya dola za Marekani milioni 36 (takribani faranga za Rwanda bilioni 47.2), uliozinduliwa Julai 2024, kwa lengo la kutoa mikopo kwa zaidi ya SME 500 kote nchini.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EADB, Bw. Benard Mono, amesisitiza kuwa Benki hiyo inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Biashara ndogo, ndogo na zile za kati (MSME) katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi ndani ya nchi wanachama, ndiyo maana imejizatiti kuimarisha upatikanaji wa huduma za kifedha na ujumuishaji wa kifedha kwa MSME. “Kwa kuwa sisi ni Benki ya maendeleo ya kikanda inayomilikiwa kwa pamoja na nchi wanachama, tunajivunia kuwa washirika wa muda mrefu wa kila nchi mwanachama, huku tukielekeza ufadhili wetu kulingana na vipaumbele vya kitaifa.

Wajibu wetu kama EADB nchini Rwanda na katika ukanda mzima si kutoa mtaji pekee, bali pia kuchochea mabadiliko ya kimfumo, ili kubadilisha fedha kuwa tija, uthabiti na fursa,” alisema Bw. Mono.

Wajumbe wa EADB

Bw. Mono ameongeza kuwa, kwa kuzingatia Dira ya Rwanda 2050, wajibu wa EADB utakuwa kufadhili kile ambacho Rwanda inapaswa kuwa kesho taifa shirikishi, lenye uthabiti na lenye ustawi kwa vizazi vya sasa na vijavyo.“Kwa pamoja, hatufadhili miradi pekee, bali tunajenga mustakabali wa Rwanda na kubadilisha maisha, mtu mmoja baada ya mwingine,” Ameongeza.

Dr James Tumusiime – EADB Board Director

Faustin Mbundu – EADB Board Director

Benki hiyo ya Maendeleo ya Afrika ya Mashariki (EADB) inao mpango wa kujenga ofisi tawi katika Mtaa wa Nyarutarama, jijini Kigali Rwanda mwaka ujao 2026 kwani wakati huu wanakodi ofisi ya kufanyia kazi.


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *