Abiola: Tunaendelea kufanya tafiti za kina ikiwemo teknolojia ya vyombo vya habari
Na Christopher karenzi
Katika Jiji la Kigali, kulifanyika mkutano wa jukwaa la kimkakati lililowaleta pamoja viongozi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ambapo walijadili masuala muhimu yatakayosaidia kuharakisha mabadiliko ya kidijitali barani Afrika.
Abiola ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa C-Suite Project Africa, inayojumuisha CAO na Tuzo za C-Suite Awards Africa.
Akizungumza katika mkutano huo, alisema: “Tunaamini kwamba hatuwezi kutoa kile ambacho hatuna. Ndiyo maana tunajikita katika kujifunza zaidi, kuimarisha uwezo wetu, na kutumia teknolojia kuleta matokeo chanya katika bara lote la Afrika. Kupitia nyaraka zetu za mapendekezo na mijadala mbalimbali, tunalenga kuwa na mchango chanya katika sera na ubunifu barani Afrika.”
Abiola Laseindeni, Mkurugenzi Mtendaji wa Edniesal Consulting kutoka nchini Nigedria , ndiye mwanzilishi na mratibu mkuu wa The CIO & C-Suite Club Africa (inayojulikana pia kama The CIO & C-Suite Project Africa). Mpango huu unajumuisha kongamano na Tuzo za C-Suite Awards Africa (The CIO & C-Suite Awards Africa), ambazo hutambua viongozi na mashirika mbali mbali. Tuzo hizi na shughuli zake huangazia utendaji bora katika sekta kama vile Fintech, AI, na mabadiliko ya kidijitali kote barani Afrika.

CEO) wa C-Suite Project Africa, Abiola Laseindeni
Aliongeza kuwa taasisi hiyo pia inaendelea kujijenga kama kituo cha tafiti na fikra (think tank). “Hii ina maana kwamba taasisi na mashirika yanapotafuta watu wenye uwezo wa kuzungumzia teknolojia, ubunifu na mageuzi ya kidijitali barani Afrika, tunataka kuwa miongoni mwa viongozi wa mbele. Tunaendelea kufanya tafiti za kina zinazogusa sekta mbalimbali, ikiwemo teknolojia ya vyombo vya habari, teknolojia ya fedha (fintech), viwanda na sekta nyingine nyingi.”
Aidha , Abiola anaeleza kuwa lengo lao kuu ni akutoa suluhisho zinazochangia ukuaji wa Afrika. “Kile tunachokipenda kufanya ni kuleta mabadiliko yenye maana na kutoa suluhisho zinazounga mkono maendeleo ya Afrika. Nilianzisha mpango huu nchini Nigeria, lakini sasa hauishii Nigeria pekee. Tunaendelea kupanua shughuli zetu katika nchi mbalimbali za Afrika, ikiwemo Rwanda.” Abiola ameongeza
Aidha, alibainisha kuwa hivi karibuni walikuwa mjini Accra, na hatua inayofuata ni kuelekea Afrika Kusini, ambapo wataendelea na mijadala kuhusu mageuzi ya kidijitali kwa ajili ya Afrika, yakiongozwa na Waafrika wenyewe.
