Makala ya 21: Kigali International Peace Marathon yarejea kwa kishindo

Share Now

Christopher Karenzi

Kwa mara ya kwanza katika historia yake, Mashindano ya Kimataifa ya Amani ya Mbio za Marathon ya Kigali (Kigali International Peace Marathon 2026), yamefanyika kwa siku mbili.

Wanariadha kutoka nchi mbalimbali wako jijini Kigali kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Kimataifa ya Amani ya Marathon ya Kigali 2026 kwa mara ya 21.  Mashindano hayo yanatarajiwa kuwakutanisha wakimbiaji wa kiwango cha juu kutoka Afrika na kwingineko duniani  katika mbio za kilomita 42.195 na km 21.097 na km10,

Zaidi ya watu 4.000 kutoka mataifa 65 duniani wameshiriki Run for Peace

Jumapili, 14 Juni 2026 kutafanyika Full Marathon na Half Marathon, macho ya mashabiki wa riadha yataelekezwa katika Uwanja wa Amahoro na barabara kuu za Kigali, ambapo maelfu ya washiriki na watazamaji wanatarajiwa kushuhudia burudani ya hali ya juu  kimataifa.

Sammy Kitwara kutoka Eldoret, Kenya  ni miongoni mwa wanariadha bora wa mwaka huu: ‘’Nimejiandaa vizuri ni mara ya kwanza kuija Rwanda nimependa hali ya hewa, ingawa kuna joto kidogo’’.

Sammy Kitwara

Kitwara  amesema kabla ya kuja Rwanda alishiriki mashindano mbali mbali lakini alipata changamoto ya baridi huko Tokyo.

Miongoni mwa wanariadha nyota wanaoshiriki mashindano ya mwaka huu ni Kigen Özbilen, mzaliwa wa Kenya mwenye uraia wa Uturuki, amesema:

 ‘’Hii ni mara ya kwanza kuja kushiriki Marathon ya Kigali, nimesikia wakisema eti Rwanda  kuna milima na mabonde, nimejitayarisha vilivyo.

Nimefanyia mazoezi kwetu Kenya na najiamini kulingana na mazoezi, Najiandaa  kupambana na wenzangu Full Marathon kilomita 42.195

Kigen Özbilen (anayejulikana kama (Kaan Kigen Özbilen) ni mwanariadha wa masafa marefu mzaliwa wa Kenya aliyebadilisha uraia na kuanza kuiwakilisha Uturuki. Alizaliwa mnamo Januari 15, 1986.

Jiji la Kigali limepokea kwa shangwe ujio wa wanariadha hao huku maandalizi ya mwisho ya Mashindano ya Kimataifa ya Amani ya Kigali (Kigali International Peace Marathon 2026) yakikamilishwa.

Kuhusu wanariadha  wanyarwanda Luteni Kanali  mstaafu Kayumba Lemuel, Rais wa Shirikisho la mchezo wa riadha nchini Rwanda, amesema marathon

Wanyarwanda ambao wamekuwa kwa muda katika kambi ya Bugesera watawasili leo. Wanakuja ili  wazoee   mazingira ya Kigali na kujiandaa kwa ajili ya kazi. Wamejiandaa vyema, tuna imani kwamba watafanya kazi yao kwa ufanisi.”

Wanariadha wa kulipwa katika makundi ya wanaume na wanawake  zaidi ya  3,870, watashiriki mashindano ya nusu marathon (Half Marathon) ya kilomita 21.09 na marathon kamili (Full Marathon) ya kilomita 42.1.

Aidha, mwaka huu, mbio za marathon kamili zitaanza saa 12:30 asubuhi, baadhi ya washiriki wa miaka iliyopita wameeleza  kuwa walikuwa wakikumbwa na changamoto ya joto la jua la Kigali katika kipindi hiki cha kiangazi. Nusu marathon ya kilomita 21 itaanza saa 8:15 asubuhi.

Mashindano yanajumuisha vipengele vitatu:

Full Marathon kilomita 42.195

Half Marathon kilomita 21.097

Run for Peace  kilomita 10 kwa washiriki wa kawaida na wanaokimbia kwa kujifurahisha

Mwaka 2025:Florence Niyonkuru alishinda medali ya dhahabu katika Half Marathon kwa wanawake.

Bigiramana Theophile alishinda medali ya shaba katika Half Marathon kwa wanaume.

Njoroge Derrick Chege alishinda medali ya dhahabu katika Half Marathon kwa wanaume.

Laban Korir alitetea ubingwa wake katika Full Marathon kwa wanaume.

Teresiah Omosa alishinda Full Marathon kwa wanawake.

Mashindano haya yanaandaliwa na Rwanda Athletics Federation kwa ushirikiano na Wizara ya Michezo, na mwaka huu yanafanyika kwa mara ya 21.


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *