Baadhi ya Waamuzi wa soka walaumiwa na Tuhuma za upangaji wa matokeo ya michezo, yameibua lawama

Share Now

Na Christopher Karenzi

Kwa muda mrefu, uamuzi  wa baadhi ya marefa umekuwa ukichafua Ligi Kuu ya Rwanda  na kusababisha kusimamishwa kwa waamuzi  huku uongozi wa Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa) ukichukua hatua.

Mwenyekiti wa APR FC, Brigedia Jenerali Deo Rusanganwa, amesema kuwa hawakuridhishwa na uamuzi wa wa marefa katika mchezo kati ya timu yake na Rutsiro FC uliofanyika kwenye Uwanja wa Umuganda jumamosi tarehe 01 Novemba 2025, akidai kwamba baadhi ya maamuzi yaliyotolewa yalionekana kuwa ya makusudi badala ya makosa ya kawaida.

Mchezo huo wa raundi ya sita ya Ligi Kuu ya Rwanda ulipigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Umuganda, na kumalizika kwa sare ya 1-1 kati ya Rutsiro FC na APR FC.

Kwa sare hiyo, APR FC imefikisha pointi 8 na kushika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi baada ya michezo sita, huku Rutsiro FC ikiwa na pointi 2 kutokana na michezo sita iliyoicheza.

Wengine wanaeleza kwamba kiwango cha mchezo kwa APR kimeshuka huku mashabiki wakieleza kuwa Kocha wao hafai.

Matatizo hayo, yakiwemo kutoka kwa mashabiki na maafisa wa soka. Baadhi ya timu zinaonyesha kutoridhishwa na maamuzi ya marefa. 

Kulingana na Nuhu ALI anatathmini kwamba tuhuma hizo zipo kweli, anaomba shirikisho  la FERWAFA kuweka adhabu kwa waamuzi ambao hawawajibiki.

Kuhusu derby  ya watani wa jadi  APR na Rayon sport itakayofanyika  amesema ‘’Ubishi umekuwa mwingi katika timu za Rwanda, kila mechi ikimalizika  wanashtaki, ikiwezekana angalau watafute waamuzi kutoka nje’’.

Aidha kuwapa mafunzo waamuzi wa ndani kuhusu jinsi ya kutumia teknolojia ya VAR kutaboresha taaluma yao, na kuoanisha mfumo wa uamuzi wa Rwanda na viwango bora vya kimataifa.

Hii haitanufaisha tu ligi ya ndani bali pia itawaandaa waamuzi wa Rwanda kwa majukumu ya kimataifa yajayo.

Hayo yakiarifiwa, Klabu ya Al Hilal SC Omdurman ni miongoni mwa timu mbili kutoka Sudan zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Rwanda (RPL) tayari wameanza mazoezi kuelekea mzunguko wa sabu wa Ligi  mkondo wa kwanza.

Timu ya Al-Hilal SC Omdurman, ambayo tayari imefuzu hatua ya makundi ya CAF Champions League, imetangaza kuwa itakuwa inachezea mechi zake za nyumbani katika Uwanja wa taifa wa  Amahoro, uwanja ambao mara nyingi ni gharama kubwa kwa timu nyingi za Rwanda.

Mwenyekiti wa Al Hilal SC,Yasir Hassan Ibrahim, amelishukuru shirikisho la FERWAFA kwa kuzipa timu hizo fursa ya kushiriki ligi ya Rwanda.Alikuwa na haya yakueleza “Tunashukuru kwa mapokezi mazuri na kwa kukubali ombi letu la kushiriki Ligi Kuu ya Rwanda.  Sisi tupo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), na tunaamini ligi hii itatusaidia katika maandalizi yetu. Hapa tunajisikia kama tuko nyumbani ”

Kocha timu ya APR FC Talib Abderrahim, kuhusu ujio wa timu hizi za Sudan, amesema kwamba ni muhimu sana kwa ligi ya Rwanda ‘’Timu hizi nazifahamu vizuri. Wachezaji wengi wa timu hizo wako katika kiwango cha juu, unapocheza na timu yenye wachezaji bora,  unapata nguvu na motisha zaidi.

Soka la Rwanda litanufaika sana. Wachezaji wetu watainua viwango vyao kwa kukutana na timu zenye viwangu bora. Namshukuru mtu aliyefanikisha ujio wa timu hizo.”

Inatarajiwa kwamba timu nyingine kutoka Sudan, Al-Merrikh, itawasili Rwanda kesho kutwa  Jumatano. Timu hizi zimeyakimbia machafuko yanayoendelea  nchini kwao Sudan.


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *