APR  BBC yatawazwa mabingwa 2025

Share Now

Timu ya mpira wa kikapu ya APR BBC imetawazwa mabingwa wa ligi kuu ya Rwanda mwaka huu 2025.

Hii ni kufuatia ushindi wa alama 81-72 dhidi ya timu ya Nishati REG baada ya kuinyuka kwa jumla ya mechi 4-1 kwenye fainali  iliyomalizika ijumaa tarehe 11 Julai 2025 katika uwanja wa BK Arena jijini Kigali, Rwanda.

Mechi zote kwa jujumla zilikuwa kali pande mbili ila APR ilikuwa makini sana na kuondoka na ushindi wa mechi 4 kwa moja kwenye mechi za fainali (Playoffs).

Hili ni taji la 3 mfululizo kwa APR, itawakiklisha Rwanda mwakani kwenye michuano ya Ligi ya Afrika  BAL 2026  itakayofanyika jijini Kigali mwakani.

APR imetwaa mataji 16 ya ubingwa: 1995, 1996, 1997, 1998, 1999, 2000, 2001, 2002, 2003, 2005, 2006, 2008 and 2009 and 2023, 2024 and 2025.

Wachezaji wa APR wakifurahia ushindi.

Kutokana na ushindi huu Timu hii imezawadiwa kombe na kitita cha faranga Milioni 15 za Rwanda.

Miaka 5 iliyopita 2009 timu zilizotwaa taji la ubingwa ni hizi zifuatazo

2025: APR

2024: APR

2023: APR

2022: REG

2021: REG

2020: Patriots

2019: Patriots

2018: Patriots

2017: REG

2016: Patriots

2015: Espoir

2014: Espoir

2013: Espoir

2012: Espoir

2011: Kigali Basketball Club

2010: Kigali Basketball club

2009: APR.

Christopher Karenzi


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *