Shema Fabrice aruhusiwa kugombea  kiti cha Urais wa FERWAFA

Share Now

Na: Mwandishi wetu Christopher Karenzi, Kigali

Shema Ngoga Fabrice amethibitishwa kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka la Rwanda (FERWAFA), katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 Agosti 2025.

Mnamo tarehe 12 Agosti 2025, Tume ya Uchaguzi ya FERWAFA ilitangaza orodha ya mwisho ya wagombea waliokubaliwa kugombea nafasi ya Urais wa shirikisho hilo.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Rugera Jean Claude, alitangaza kuwa mgombea pekee aliyekubaliwa kugombea ni Shema Ngoga Fabrice, baada ya Hunde Walter, ambaye awali alionyesha nia ya kugombea, kujiondoa dakika za mwisho.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Rugera Jean Claude, amethibitisha kuwa Shema Fabrice ndiye mgombea pekee kwa nafasi ya Urais wa FERWAFA.

Kwa upande mwingine, baadhi ya waliokuwa kwenye orodha ya waliopendekezwa na Hunde – ambao ni Rurangirwa Louis na Ngendahayo Vedaste, wanachama wa Kamati Tendaji ya FERWAFA – waliiandikia Tume ya Rufaa ya Uchaguzi wakiomba kuondolewa kwa Shema Fabrice kabla ya jina lake kuthibitishwa rasmi.

Mwenyekiti wa Tume ya Rufaa ya Uchaguzi katika FERWAFA, Me Gasasira Jafari, alisema:
“Wanaume hawa walikata rufaa kama wajumbe wa Kamati Tendaji, hivyo hawakuwa na mamlaka ya kisheria kufanya hivyo, kwani mamlaka hayo ni ya kiongozi mkuu au mgombea mwenyewe. Kwa hivyo, tulibaini kuwa hawakuwa na haki ya kukata rufaa hiyo.”

Mwenyekiti wa Tume ya Rufaa ya Uchaguzi katika FERWAFA, Me Gasasira Jafari

Hata hivyo, ombi hilo lilikataliwa kwa kuwa Tume ya Rufaa ya Uchaguzi ilibaini kuwa waliowasilisha rufaa hiyo hawakuwa na mamlaka ya kisheria kufanya hivyo.

Inatarajiwa kuwa kampeni za uchaguzi zitaanza tarehe 13 hadi 29 Agosti 2025, kabla ya uchaguzi rasmi kufanyika tarehe 30 Agosti 2025.

Orodha ya watu watakaofanya kazi na Shema Fabrice iwapo atachaguliwa ni:

  • Mugisha Richard – Makamu wa Kwanza wa Rais
  • Me Gasarabwe Claudine – Makamu wa Pili wa Rais
  • Nshuti Thierry – Kamishna wa Fedha
  • Niyitanga Désiré – Kamishna wa Mashindano
  • Gicanda Nikita – Kamishna wa Soka la Wanawake
  • Me Ndengeyingoma Louise – Kamishna wa Masuala ya Sheria
  • Lt Col Mutsinzi Hubert – Kamishna wa Huduma za Afya
  • Hakizimana Louis – Kamishna wa Masuala ya Waamuzi

Baadhi ya watu watakaofanya kazi na Shema Fabrice iwapo atashinda uchaguzi.


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *