APR yatawazwa Mabingwa wa ligi msimu 2022-2023
Timu ya APR FC imetawazwa mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Rwanda kwa mara ya 21 msimu wa 2022-2023.
Kulikuwa na ushindani wa hali ya juu msimu huu kwasababu kati ya APR na Kiyovu Sports Club, timu zote zimemaliza zikiwa sambamba kwa alama 63 kwa jumla ya mechi 30 ila timu hii ya jeshi la Rwanda APR, wamefunga magoli mengi wana akiba ya magoli 24 huku Kiyovu wakiwa ana akiba ya magoli 14. Kulingana na Shirikisho la soka nchini Rwanda FERWAFA, timu zikiwa sare kwa alama anayebeba kombe ni yule aliyefunga magoli mengi.
Mashabiki wa Apr wamefurahia ubingwa huu wa nne mfululizo na vikombe 21 kwa jumla tangu mwaka 1995.

APR wakifurahia ubingwa
Kocha mkuu wa APR Ben Moussa alikuwa na haya ya kueleza kuhusu ligi kuu iliyomalizika Mei 28, 2023. Kocha Mousa amesema ‘’Mwaka huu timu zote zilipewa fursa ya kutumia wachezaji wa kigeni kuliko mwaka jana. Kila timu ilikuwa na uwezo wa kutumia wachezaji wa kigeni 5, yaani kiwango cha soka kilipanda, ilikuwa ni vigumu kidogo kwetu. Tulionyesha kwamba wachezaji wetu mzawa, APR wapo mabingwa mara nne mfululizo’’.
Wapinzani wengine ni Rayon sport yenye mashabiki wengi nchini na nje wamemaliza kwenye nafasi ya 3 wakiwa na alama 61.
Timu ya Rutsiro na Espoir FC zimeshuka daraja la pili wakati timu ya Etoile de l’Est na Amagaju FC zikia zimepanda daraja la kwanza.
Timu hiyo ya APR pamoja na mashabiki wao wakiwa kwenye Bus la Tembera u Rwanda (Visit Rwanda), wamepata fursa ya kutembezwa jiji la Kigali jana jioni kabla ya kuelekea kambini kujiandaa fainali ya kombe la Amani kukabiliana na mtani wake Rayon juni 03, 2023 mjini Huye kusini mwa Rwanda.
Mahabaiki wa APR walianzia safari yao Kigali Pelé Stadium, Nyamirambo kuri 40, Biryogo mtaa wa Gitega, soko kuu la Nyarugenge, Kigali City Tower, City Plaza, CHIC, Yamaha, Nyabugogo, Giti cy’Inyoni, hadi Shyorongi kwenye makao ya timu hiyo.





Christopher Karenzi
