Dr.Vincent Duclert: Utafiti juu ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwaka 1994 utaendelea

Share Now

Kongamano la  kimataifa la siku 9 lililokuwa likifanyika  nchini Rwanda kuhusu utafiti wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya watutsi, umetamatika jumatatu tarehe 19 Septemba 2022. Washiriki  wa Kongamano hili wameazimia kuendelea kufanya utafiti juu ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwaka 1994.

Miongoni mwa walioshiriki kwenye kongamano hilo la siku tisa ni Mwanahistoria kutoka nchini Ufaransa Dr. Vincent Duclert, aliyeongoza uchunguzi kubaini ushiriki wa Ufaransa, kuhusu mauaji hayo, yaliyosababisha vifo vya watu Milioni moja, kwa kipindi cha miezi mitatu. 

Kongamano hilo  liliandaliwa na Tume ya  Duclert  kwa ushirikiano na Wizara ya Umoja na maridhiano ya Rwanda, Chuo kikuu cha Rwanda tawi la Huye  kusini mwa nchi   pamoja na mashirika mbali mbali ikiwa ni pamoja na jumuiya ya manusura  wa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda IBUKA.

Na hapa namkuuu ‘’Tumeazimia  kuendelea na utafiti, ripoti ya tume yangu ni ripoti ya utafiti na kwa hivo hatukuweka bidii ya kufanya utafiti kuhusu nafasi ya Ufaransa, kwasababu nafasi yake inajulikana.  Tumejikita juu ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi nchini Rwanda’’.

Mwanahistoria Dr.Vincent Duclert

Dr, Duclert, Aliyeongoza tume ya wanahistoria iliyoundwa nchini Ufaransa kuchunguza ushiriki wa nchi hiyo kwenye mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994, amesema kwamba walifikiria Kongamano la siku 9 mjini Kigali pamoja na Kampasi ya  Chuo kikuu cha Huye  ili kujadiliana umuhimu wa  suala la mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi, ilitakiwa kuhamasisha zaidi watafiti 100 kwa muda wa siku 9.

Egide Nkuranga, ni mwenyekiti  wa  Jumuiya ya manusura  wa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda  IBUKA amesema kwamba kuna mambo  mengi hayajafanyiwa utafiti, wamejadiliana kuhusu  faili za kumbukumbu za IBUKA ambazo ziko sehemu mbali mbali.

Amebaini kuwa wazo lililojitokeza ni kwamba kuna baadhi ya watu binafsi wana  faili zingine ambazo hazijafanyiwa utafiti. Amesema  ‘’Kuna mambo mengi  tena mengi  hayajafanyiwa utafiit. Kuna nyaraka  mbali mbali  ziko hapa na pale,  wamekuja ofisini Ibuka  tumewaonyesha tunayoyafanya ikiwa ni pamoja na nyaraka, pia kuna baadhi ya watu binafsi wana faili ambazo hazijafanyiwa utafiti’’.

Hizo faili zitasaidia watafiti hao kupata habari zinazohitajika juu ya mauaji ya kimbari.

Mwanasheria Tite Gatabazi  ni mmoja wa wadau  wa kongamano hili  amesema kuna ujumbe wa  rais Macron wa Ufaransa  unaambatana na ujumbe wa  rais Paul Kagame, inabidi eti  ukweli wa mauaji ya kimbari  dhidi ya watutsi ujulikane

Inabidi hivi sasa  tueleze ukweli wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini isiwe kusema mambo watu haajui

Gatabazi ameongeza kuwa katika mazungumo yao, kuna mpango wa kujenga maktaba ya kimataifa  itakayojengwa hapa Rwanda kwa ushirikiano wa Kigali na Ufaransa  ili kutoa elimu kwa wenyeji, wageni na watafiti kuhusu  mauaji hayo.

  • Dr. Bizimana Jean Damascene waziri wa Umoja katikati kutoka kulia, Antoine Anfré Balozi wa Ufaransa wa pili katikati kutoka Kushoto.

Karenzi Christopher


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *