Dr.Vincent Duclert: Utafiti juu ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwaka 1994 utaendelea
Kongamano la kimataifa la siku 9 lililokuwa likifanyika nchini Rwanda kuhusu utafiti wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya watutsi, umetamatika jumatatu tarehe 19 Septemba 2022. Washiriki wa Kongamano hili wameazimia kuendelea kufanya utafiti juu ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwaka 1994.
Miongoni mwa walioshiriki kwenye kongamano hilo la siku tisa ni Mwanahistoria kutoka nchini Ufaransa Dr. Vincent Duclert, aliyeongoza uchunguzi kubaini ushiriki wa Ufaransa, kuhusu mauaji hayo, yaliyosababisha vifo vya watu Milioni moja, kwa kipindi cha miezi mitatu.
Kongamano hilo liliandaliwa na Tume ya Duclert kwa ushirikiano na Wizara ya Umoja na maridhiano ya Rwanda, Chuo kikuu cha Rwanda tawi la Huye kusini mwa nchi pamoja na mashirika mbali mbali ikiwa ni pamoja na jumuiya ya manusura wa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda IBUKA.
Na hapa namkuuu ‘’Tumeazimia kuendelea na utafiti, ripoti ya tume yangu ni ripoti ya utafiti na kwa hivo hatukuweka bidii ya kufanya utafiti kuhusu nafasi ya Ufaransa, kwasababu nafasi yake inajulikana. Tumejikita juu ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi nchini Rwanda’’.

Dr, Duclert, Aliyeongoza tume ya wanahistoria iliyoundwa nchini Ufaransa kuchunguza ushiriki wa nchi hiyo kwenye mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994, amesema kwamba walifikiria Kongamano la siku 9 mjini Kigali pamoja na Kampasi ya Chuo kikuu cha Huye ili kujadiliana umuhimu wa suala la mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi, ilitakiwa kuhamasisha zaidi watafiti 100 kwa muda wa siku 9.
Egide Nkuranga, ni mwenyekiti wa Jumuiya ya manusura wa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda IBUKA amesema kwamba kuna mambo mengi hayajafanyiwa utafiti, wamejadiliana kuhusu faili za kumbukumbu za IBUKA ambazo ziko sehemu mbali mbali.
Amebaini kuwa wazo lililojitokeza ni kwamba kuna baadhi ya watu binafsi wana faili zingine ambazo hazijafanyiwa utafiti. Amesema ‘’Kuna mambo mengi tena mengi hayajafanyiwa utafiit. Kuna nyaraka mbali mbali ziko hapa na pale, wamekuja ofisini Ibuka tumewaonyesha tunayoyafanya ikiwa ni pamoja na nyaraka, pia kuna baadhi ya watu binafsi wana faili ambazo hazijafanyiwa utafiti’’.
Hizo faili zitasaidia watafiti hao kupata habari zinazohitajika juu ya mauaji ya kimbari.
Mwanasheria Tite Gatabazi ni mmoja wa wadau wa kongamano hili amesema kuna ujumbe wa rais Macron wa Ufaransa unaambatana na ujumbe wa rais Paul Kagame, inabidi eti ukweli wa mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi ujulikane
Inabidi hivi sasa tueleze ukweli wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini isiwe kusema mambo watu haajui
Gatabazi ameongeza kuwa katika mazungumo yao, kuna mpango wa kujenga maktaba ya kimataifa itakayojengwa hapa Rwanda kwa ushirikiano wa Kigali na Ufaransa ili kutoa elimu kwa wenyeji, wageni na watafiti kuhusu mauaji hayo.

- Dr. Bizimana Jean Damascene waziri wa Umoja katikati kutoka kulia, Antoine Anfré Balozi wa Ufaransa wa pili katikati kutoka Kushoto.
Karenzi Christopher
