Mpira wa wavu: Washiriki wa Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika watembelea Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari ya Kigali

Share Now

Na Karenzi Christopher

Viongozi, wachezaji, makocha, waamuzi wa kimataifa pamoja na wasaidizi wa timu wanaoshiriki mashindano ya CAVB Men’s Club Championship 2026, yanayozikutanisha timu bingwa za mpira wa wavu barani Afrika   ambayo  yanayofanyika nchini Rwanda, jumanne  tarehe 28 April 2026 wametembelea Jengo la Makumbusho  ya Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi ya mwaka 1994. eneo la Gisozi jijini Koigali na kutoa heshima kwa wahanga waliopumzishwa hapo.

Tukio hilo lilifanyika Jumanne, tarehe 28 Aprili 2026, na lilihudhuriwa na wawakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Rwanda (FRVB), Shirikisho la Mpira wa Wavu Afrika (CAVB), pamoja na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Wavu (FIVB).

Wametembelea sehemu mbalimbali za kumbukizi na kuelezwa jinsi mauaji ya kimbari yalivyopangwa na kutekelezwa, pamoja na safari ya miaka 32 ya ujenzi upya wa Rwanda baada ya kutoka katika giza la mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi, yaliyositishwa na jeshi la RPA-Inkotanyi.

Rais wa FRVB, Ngarambe Raphaël, amesema kuwa ushiriki wa timu katika mashindano ya Afrika ya klabu za wanaume ni ishara ya umoja wa Waafrika.

Amesema: “Tumeandika ujumbe (kwenye kitabu cha wageni) unaotutia moyo, wakisisitiza kuwa wanatamani jambo hili lisitokee tena. Tukio hili linaonyesha nafasi ya michezo katika maisha ya binadamu. Michezo imeonyesha kuwa watu wanapaswa kushirikiana ili mauaji ya kimbari yasitokee tena.”

Aidha, Ngarambe amewataka wanamichezo wote kuendelea kukumbuka historia ya Rwanda na kujitahidi kuhakikisha haitajirudia, huku akiwahimiza vijana kupambana na itikadi ya mauaji ya kimbari.

Mwakilishi wa Shirikisho la mchezo wa Voliboli duniani, FIVB kutoka Uganda, Shilla Omuriwe Buyungo, amesema kuwa ubinadamu ulishindwa na kuruhusu mauaji ya kimbari kutokea.

Amesema: “Hatuwezi kuchagua mahali pa kuzaliwa au sisi ni nani; hilo ni la Mungu. Nilichojifunza hapa ni kwamba tunapaswa kueneza upendo. Mpende mtu uliyenaye kwa sababu hachagui kuwa vile alivyo. Kupendana ndiko Mungu anatutaka.”

Amesisitiza kuwa michezo inapaswa kuwa chombo cha kukuza mazungumzo na kuimarisha upendo ili kuhakikisha yaliyotokea hayatokei tena.

Kumbukizi ya Mauaji ya Kimbari ya Kigali imehifadhi miili ya zaidi ya Watutsi 259,000 waliouawa wakati wa mauaji hayo, kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Kigali na viunga vyake.

Mashindano ya CAVB Men’s Club Championship 2026 yanaendelea Jumatano tarehe  29 Aprili 2026 kwa michezo ya hatua ya 16 bora pamoja na ile ya kuwania nafasi za 17 hadi 24, katika toleo la 47 la mashindano hayo.


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *