Mutobo:Zaidi ya watu 214 wahitimu masomo ya kizalendo na historia ya Rwanda

Share Now

Christopher Karenzi

Naibu Msemaji wa Serikali ya Rwanda, Uwera Jean Maurice, amewataka waliokuwa wanajeshi wa zamani wa FDLR, waliorejea  nchini Rwanda kutoka mashariki mwa DRC kuthamini fursa waliyopewa ya kuitwa tena raia wa Rwanda baada ya miaka  wakiwa katika misitu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC

Uwera aliyasema hayo Jumnanne tarehe 30 Machi 2026 akiwa  katika kituo cha Mutobo kinachopokea wanaorejea kutoka DRC.

Tume ya Taifa ya kuwaaga na kuwarejesha katika maisha ya kawaida waliokuwa wanajeshi wa zamani RDRC, imewaga rasmi kundi  la waliokuwa wanachama wa makundi yenye silaha  Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikiwemo FDLR ambao wamemaliza miezi mitatu katika kituo cha Mutobo kinachowapokea, Wilaya ya Musanze, mkoa wa kaskazini mwa Rwanda.

Katika awamu hii, 214 wamehitimu masomo ya kizalendo na kujua historia ya Rwanda, huku tume hiyo ikitangaza kuwa kuna wengine 400 walio tayari kuanza mafunzo ya kuwawezesha katika maisha ya kawaida, katika kundi la 77.

Naibu Msemaji  wa Serikali ya Rwanda, Uwera Jean Maurice, amesema kuwa kundi la kigaidi la FDLR bado lipo na linaendelea nchini DRC:

 “Ninakuhakikishia kwamba FDLR bado ipo, na katika miaka ya hivi karibuni imeendelea kuimarika kwa kiasi kikubwa.

  Hali hii inahusishwa na serikali ya Tshisekedi, ambayo inashutumiwa kuwa na itikadi ya mauaji ya kimbari pamoja na matumizi ya lugha ya chuki, kauli zinazolenga kusaidia serikali ya Kinshasa kuendelea kubaki madarakani’’. Amesema

Aidha amewataka  waliorejea nchini kuthamini fursa waliyopewa ya kuitwa tena Wanyarwanda baada ya miaka 31 wakiwa katika misitu ya DRC.

Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya kuwaaga na kuwarejesha katika maisha ya kawaida waliokuwa wanajeshi wa zamani, Nyirahabineza Valerie, amesema kuwa miongoni mwa waliorejea nyumbani, waliokuwa wanajeshi ni 178, wakiwemo wanawake saba.

Amesema siku hizi wanaorejea ni wengi kuliko awali kama anavyoeleza amesema: Siku hizi tunapokea watu wengi zaidi ikilinganishwa na wale tuliokuwa tunapokea hapo awali. Wengi wao wanapofika hapa wakia wametoroka,  eti wanajificha katika jamii huko Goma.

Kuja Rwanda wanaona ni rahisi kwao.  wanapofika kwa M23 hawauawi, hawapigwi, wala hawarudishwi walikotoka. Ndivyo wanavyotuambia; badala yake wanaachwa na  kurudi Rwanda’’.

Bi  Nyirahabineza,  ameongeza kuwa tangu kuanza kwa programu ya kuwafundisha na kuwaandaa waliokuwa katika makundi yenye silaha kama FDLR wanaorejea nyumbani hupitia kituo cha Mutobo ambapo  kuna jumla ya watu 12,686 waliorejea  kwenye familia zao.

Aidha amewaasa kuwa na ushirikiano: “Tarafa zote hizi zinapakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jambo linalorahisisha kwa vijana kushawishiwa na FDLR au kutumiwa wajumbe, na kuvuka mpaka kwa urahisi sana. Ndiyo maana tunahitaji ushirikiano wa Wanyarwanda wote ili kuwahamasisha vijana kupuuza wanaowashawishi.”

Miongoni mwa waliorejeshwa katika maisha ya kawaida, watu 162 wanatoka Wilaya ya Rubavu, tarafa za Mudende, Bugeshi, Gisenyi, Nyamyumba, Busasamana, Cyanzarwe, Kanama na Kanzenze Tarafa ya Mudende ndiyo ina idadi kubwa zaidi ya watu, ikiwa na watu 33.


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *