Emmanuel Okwi : Hakuna muda wa kulegeza unapocheza soka

Share Now

Emmanuel Okwi ni mchezaji  maarufu wa soka  kutoka nchini  Uganda akiwa amesajiliwa na Club ya AS Kigali hapa nchini Rwanda. Alicheza katika vilabu mbali mbali barani  Afrika na Ulaya . Nimefanya mahojiano naye, nimeanza kumuuliza Okwi ni mtu gani?

Emmanuel Okwi : Kwanza kabisa ni mchezaji anayeogopa Mungu, ni mtu ambaye anajituma  siku zote uwanjani, kila nafasi anayopata anahakikisha  kwamba anapambana, anaisadia timu yake anayoichezea na vile vile kuungana na wenzake na kufanya kazi kwa pamoja.

Brightafrica.rw: Umecheza katika timu mbali mbali, leo upo katika kikosi cha AS Kigali timu ya jiji la Kigali, mkataba wako na Club  ni wa muda gani?

Emmanuel Okwi :  AS Kigali, nimesaini mkataba wa mwaka mmoja  wakati huu ndo tunaingia wa pili wa ligi kuu msimu huu wa 24/2025, kwa wkati huu  bado nina miezi 6 kwenye mkataba wangu.Niko kwa ajili ya kusaidia timu yangu kuhakikisha inamalizia kwenye nafasi nzuri kwenye ligi na kombe la Amani.

Brightafrica.rw: Ulisajiliwa wakati ligi tayari ilianza  mapema mwaka jana na wewe ni miongoni mwa wafungaji bora kwenye  mzunguko wa Kwanza wa ligi, una siri gani ya kupachika mabao langoni?

Emmanuel Okwi : Ehh unajuwa siku zote ni kuungana na wenzio, ukiwa na wachezaji wazuri , mfano katika timu yetu tuna wachezaji wazuri wanaojituma, wanapambana lakini pia namshukuru Mungu kwasababu sikuwa na pre season  nzuri , hata hivo mambo hayajawa mabaya.

 Nashukuru Mungu. So… ni hivo  kujituma na  kuhakikisha  ukipata nafasi unaitumia.

Brightafrica.rw:  Ligi kuu ya soka  ya Rwanda msimu huu wa 2024/25 unaionaje labda  tofauti na ligi zilizopita ?

Emmanuel Okwi:  Ligi ni ngumu kwa sababu wameongezeka wachezaji wa kigeni, ushindani unakuwa juu zaidi ndo maana timu hazijaachana sana kwa pointi nyingi timu ni kama zinalingana nguvu. Msimu wa 2021/22 nilipokuwa hapa kuna tofauti kidogo, msimu huu ni mgumu sana lakini ni vizuri pia ili kuinua viwango vya wachezaji.

Hakuna muda tena wa kulegeza kuhisi kwamba mambo ni mepesi, lazima ujitume kila siku na uhakikishe unapata nafasi ya kucheza usipojituma ndo hivo utakuwa unakaa nje.

Brightafrica.rw: Mbali na AS Kigali  nitajie timu  zingine ulizowahi kuchezea.

Emmanuel Okwi: Nilianzia Villa Sports Club katika timu ya watoto (junior) nilipanda  hadi timu  kubwa ya Villa nchini  Uganda, halafu nikasajiwa na Simba SC, baadae Etoile du Sahel ya Tunisia ; sijakaa sana pale  kutokana na mambo mbali mbali  nikarudi Simba baadae nikaondoka na kuelekea Denmark.

Okwi ameeleza orodha ya timu nyingine huko Uganda, kacheza msimu mmoja baadae akaelekea Yanga, akarudi tena Simba ambako alicheza kwa kipindi kirefu. Alimaliza mkataba wake 2019 katika club hiyo ya Msimbazi.

Baadae alisafiri hadi Misri, alicheza misimu miwili baadae alisajiliwa na Club ya Kiyovu  kisha akaelekea nchini Iraq, alovomaliza mkataba huko alirejea nyumbani Uganda halafu  baadae alipata usajili wa AS Kigali msimu huu.

Brightafrica.rw: Baada ya safari hiyo ndefu  nieleze sasa mafanikio licha ya kwamba bado upo kwenye soka  :

Emmanuel Okwi: Mafaniko ambayo naweza kusema zaidi, nimejifunza vitu vingi , nimejifunza tamaduni na mila mbali mbali ukiachana na mapato yaani pesa. Ni vitu nadhani vitanisaidia hata nikimaliza kucheza mpira , itanisaidia  kuwa mkufunzi  wa maisha ya baadae na nashukuru Mungu sana kwa hilo.

Okwi  alitawazwa kuwa mchezaji bora wa kigeni mara 2 katika ligi kuu ya soka akiwa kwenye club ya Simba, Tanzania Amesema ndoto zake ni kuwa Kocha ili asaidie vijana kucheza soka, ujuzi alionao ni mwingi. Amebaini kuwa ikiwa hilo halitowezekana anataraji  siku za usoni kufanya kazi ya kusaka wachezaji wazuri kucheza kwenye vilabu vya soka.

Brightafrica.rw: 

Kwenye ukanda huu ni wachezaji gani  mashuhuri huwezi kuwasahau walipokuwa wakicheza mpira mpaka na wewe unafurahia kuwaona.

Emmanuel Okwi: Of course ukiangalia..  Fiston Mayele wa DRC , ukiangalia Haruna Niyonzima hapa Rwanda  pia na huko Tanzania alikuwa maarufu sana, Afrika Mashariki nadhani wanamjuwa, wengine ni Chama wa Zambia,  tulicheza naye katika timu ya  Simba, yupo Meddy Kagere  mnyarwanda mwenye asili ya Uganda na John Bocco wa Tanzania, ni wengi lakini hao siwezi kuwasahau.

Brightafrica.rw:   Ni mchezaji gani  wa kimataifa aliyekuvutia zaidi kumpenda wakati ukiwa mdogo?

 Emmanuel Okwi: Ni mchezaji mmoja tu Thierry Henry  wa Arsenal huyo  nilimpenda sana  kwa uchezaji wake nilipokwa mdogo.  Wakati naanza kucheza nilivaa jezi Namba yake.

Bado nampenda huenda siku moja tutakutana huwezi kujuwa kwenye mambo yetu ya mpira. Na pia mimi  ni mpenzi wa Arsenal.

Brightafrica.rw:   Kwa kumalizia unapenda  kula chakula gani? 

Emmanuel Okwi: Napenda wali na maharage na ugali pia hapo najihisi vizuri.

Brightafrica.rw:   Nashukuru kwa wakati wako.

 Emmanuel Okwi: Asante

Christopher Karenzi


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *