Al Hilal SC Ombdurman yatinga hatua ya ¼ Finali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Na Christopher Karenzi.
Timu ya Al Hilal SC Ombdurman ya Sudan imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la CAF Champions League na kuwashukuru Wanyarwanda kwa sapoti yao kubwa katika mashindano hayo mwishoni mwa juma.
AL Hilal imefikia hiyo baada ya kuwafunga Saint-Éloi Lupopo bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa wa Amahoro jijini Kigali.Mchezo huo ulihudhuriwa na mashabiki wengi kwani uliunganishwa na mchuano wa Ligi Kuu ya Rwanda kati ya APR FC na Kiyovu Sports. Pia ulikuwa ni mchezo wa mwisho wa Kundi C katika mchuano wa Ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF Champions League).
Kwa msimamo wa kundi C, Al Hilal SC Ombdurman wamemaliza michuano ya makundi wakiongoza kwa alama 11, nafasi ya pili ni Mamelodi Sundowns ya Afrika ya Kusini, wamemaliza kwa alama 9 wakati MC Alger ya Algeria wakiwa na alama 7hatimayeSaint-Éloi Lupopo kutoka DRC wanashikilia mkia na alama 5.

Wakati Al Hilal wakisherehekea hatua waliyofikia ya kutinga robo fainali ya mashindano haya yanayokutanisha vilabu vikubwa barani Afrika, na baada ya kuizidi nguvu miamba mingine ikiwemo Mamelodi Sundowns, mashabiki walikuwa wakitamka kwa furaha: “Asante Rwanda.”
Maneno hayo pia yalionekana kwenye mabango yaliyokuwa yakishikiliwa na raia wa Sudan wanaoishi Rwanda, wakionesha kuwa nchi hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya timu yao, huku Wanyarwanda wengi wakiendelea kuipa sapoti. Ujumbe huo ulitolewa kupitia mitandao ya kijamii ya klabu hiyo usiku wa Jumamosi, tarehe 14 Februari 2026

Al Hilal SC yaishukuru Rwanda kwa sapoti ya mashabiki kwenye mashindano ya kimataifa
Al Hilal SC ni moja ya timu za Sudan zinazoshiriki Ligi Kuu ya Rwanda kutokana na changamoto za kiusalama zinazoendelea nchini kwao, na imekuwa ikicheza mechi zake za kitaifa na kimataifa jijini Kigali.

Wachezaji wa Al Hilal SC wakifurahia bao la ushindi
Baada ya mchuano huo wa kimataifa, ilifuata mechi ya ligi kuu ya soka baina ya watani wa jadi Kiyovu Sports Club na APR FC. Hadi kipenga mwisho kupulizwa timu hizo zilimaza kwa sare bao 1-1 katika uwanja wa Amahoro. Nuru Ali anatathmini kuhusu mchuano huo
Hayo yakijiri jumanne hii tarehe 17 Februari 2026, ni kidumbwendumbwe ambapo mashabiki wa Rwanda watashuhudia dabi kati ya Al Merrikh na Al Hilal Omdurman kwenye Ligi kuu ya soka itakayofanyika kwenye uwanja wa taifa wa Amahoro, jijini Kigali.
