Tanzania: Rais Samia Suluhu Hassan ameteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi

Share Now

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) siku ya Jumapili, Januari 19, kwa kauli moja wamemteua Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wao kutetea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.

Makamu huyo wa zamani wa rais, aliyechukua nafasi ya Rais John Magufuli, aliyefariki dunia ghafla mweziMachi 2021, alionyesha dalili za uwazi alipoingia madarakani, hasa akiidhinisha vyombo vya habari vilivyopigwa marufuku na mtangulizi wake kurudi kufanya kazi. Lakini upinzani umemtuhumu katika miezi ya hivi karibuni kurejea kwenye vitendo vya John Magufuli (watu kukamata, kutekwa n.k.)

CCM ilifanya mkutano mkuu usio wa kawaida siku ya Jumamosi na Jumapili kumchagua makamu wa rais wa chama hicho na kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani kwa miaka minne iliyopita.

Hatimaye wanachama hao walitaka na kupata ridhaa ya Bi Hassan na Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi kuwa wagombea wao kutetea tena nafasi za urais katika uchaguzi wa mwezi Oktoba.

“Hatuna wagombea mbadala kwa mwaka 2025,” iliandikwa kwenye mabango. “Tumetimiza mengi katika miaka minne iliyopita na ninaahidi kufanya mengi zaidi katika muhula ujao,” rais Smia Suluhu Hassan alisema. “Ninaomba kila mtu kudumisha umoja wetu tunapokaribia uchaguzi,” aliongeza katika hotuba yake ya kufunga kikao cha CCM.

Wiki iliyopita, kiongozi wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT Wazalendo), Dorothy Semu, alitangaza nia yake ya kukabiliana na Bi Hassan katika uchaguzi wa mwezi Oktoba. Chama kikuu cha upinzani cha Chadema bado hakijaanza mchujo huu, lakini kinatarajiwa kumchagua rais mpya siku ya Jumanne.

Hata hivyo, chama hicho kilionya mwishoni mwa mwaka 2024 kuhusu nia yake ya “kuzuia” uchaguzi wa mwaka 2025 ikiwa mageuzi makubwa ya mfumo wa uchaguzi hayatatekelezwa kufikia wakati huo. Ombi la muda mrefu, lililopuuzwa mara kwa mara na chama tawala.

Tangazo hili limekuja baada ya matokeo ya uchaguzi wa ndani ya Novemba 27, uliochakachuliwa kwa mujibu wa Chadema, hali ambayo ilionyesha CCM ikipata ushindi mkubwa.

Source : RFI


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *