Mfaransa Bruno Ferry ateuliwa kuwa kocha mkuu wa Rayon Sports

Share Now

Na Christopher Karenzi

Kocha Mfaransa Bruno Ferry ameteuliwa rasmi kuwa kocha mkuu wa Rayon Sports. Taarifa hiyo ilitangazwa na klabu hiyo jioni ya Jumatano, tarehe 17 Desemba 2025, kupitia mitandao yake ya kijamii.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58anatarajiwa kuwasili mjini Kigali siku ya Ijumaa, ambapo atasaidiwa na makocha wasaidizi Lomami Marcelna Haruna Ferouz.

Rayon Sports ilikuwa haina kocha mkuu tangu Novemba 2025, baada ya kumfuta kazi Afhamia Lotfi kutokana na matokeo duni ya timu.

Bruno Ferry anamiliki leseni ya ukocha ya UEFA Pro (Daraja A) na ana uzoefu mkubwa wa kufundisha barani Afrika. Amewahi kuzifundisha klabu kadhaa zikiwemo AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Azam FC ya Tanzania na Accra Lions ya Ghana.

Rayon Sports haijaanza vyema msimu huu wa ligi, ambapo kwa sasa inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 17, ikiachwa kwa pointi tisa na vinara Police FC.

Kocha Mfaransa Bruno Ferry

Klabu hiyo tayari imeanza mchakato wa kusajili wachezaji wapya watakaojiunga na timu katika dirisha la usajili la Januari 2026, kwa lengo la kuboresha matokeo. Miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa ni Muganda Muhamed Kagawa Ssenoga, aliyekuwa akiichezeaExpress FC ya Uganda.

Rayon Sports inarejea dimbani Ijumaa, tarehe 19 Desemba 2025, itakapokuwa mgeni wa Gorilla FCkatika mchezo wa siku ya 12 ya Ligi Kuu.


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *