Tadej Pogačar, aandika historia ya kutwaa medali ya dhahabu Rwanda, barani Afrika
Christopher Karenzi
Nyota huyo kutoka Slovenia Tadej Pogačar alimaliza mbio za kilomita 267.5 kwa muda wa saa 6 dakika 21 na sekunde 20. Amevikwa medali ya dhahabu na Rais wa Rwanda Paul Kagame
Mbelgiji Remco Evenepoel, aliyemshinda kwenye mbio za “Time Trial” zilizofanyika Septemba 21, alimaliza nafasi ya pili kwa kutofautiana dakika moja na sekunde 26 na bingwa huyo wa dunia.
Tadej ameeleza furaha yake ‘’Ndiyo, ilikuwa ni uzoefu mzuri sana kuja hapa. Wiki iliyopita kulikuwa na “Time Trial,” kulikuwa na changamoto kadhaa lakini tuliweza kudhibiti. Wiki hii tumefanya mbio nzuri sana pamoja na timu, ilikuwa ya kufurahisha kweli. Nimefurahi sana nimeweza kushinda’’.

Rais Kagame akimtunuku mshindi Tadej Pogačar medali ya dhahabu
Kati ya waendesha baiskeli 165 walioanza shindano gumu la jana, ni 31 pekee waliomaliza na hakuna Munyarwanda aliyefanikwa kumaliza licha ya washiriki sita kuingia kwenye mashindano haya.
Ilikuwa ni furaha kuona wawakilishi kutoka mataifa mbali mbali ya Afrika , Ethiopia, Uganda , Tanzania, Eritrea, timu kutoka Ulaya, Marekani , Asia…….. Watu mbali mbali wametoa hisia zao kuhusu mashindano haya ya mbio za dunia. Mashindano haya yalikuwa magumu, kama wanavotoa hisia zao..
Shabiki mnyarwanda kutoka jijini Kigali, amewaasa wenyeji kutokata tamaa kutokana na kushindwa kufanya vizuri kwenye mashinano haya makubwa.
Amesema ‘’Wanyarwanrwanda naendelea kuwapa pole hamkufika mbali iwezekanavyo, siku zijazo tunaweza kukufanya vizuri, niwambie wanyarwanda kuwa wiki nzima tumefurahi ‘’
Rais wa Rwanda Paul Kagame amefurahia kiwango cha wachezaji na hamasa kwa jumla. ‘’ Tangu siku ya kwanza ya shindano hili, lilileta furaha isiyo ya kawaida na nguvu za aina yake kwenye mitaa ya Kigali’’
Ameongeza ‘’Badhi ya wachezaji wenye vipaji duniani wamefanya maajabu kwa viwango vya juu. Hii ni storia imeandikwa barani Afrika yote kwa namna ya pekee kwa Rwanda’’ Amesema Rais Kagame
Gabriel Landa ni Kocha msaidizi wa timu ya Tanzania ya Mbio za baiskeli amesema kwamba mashindano yalikuwa ni changamoto kwao lakini pia ni kujifunza ’’Wachezaji wengi ni mara yao ya kwanza kushiriki mashindano makubwa kama haya’’.
Ameongeza kuwa ‘’ Tangu yalipoanza mashindano haya tumeshindwa kushika zile nafasi nzuri wale wote walioweza kumaliza nawapongeza’’ Amesema Landa.
Mashindano hayo yalianza tarehe 21 Septemba na kutamatika tarehe28 Septemba 2025.

Aidha Mfaransa David Lappartient amechaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho la Kimataifa la mbio za baiskeli duniani (UCI) kwa miaka minne ijayo, ambapo muhula wake utamalizika mwaka 2029.
Uchaguzi wa Rais wa UCI umefanyika katika Mkutano wa 194 wa UCI uliofanyika jijini Kigali wiki iliyopita tarehe 25 Septemba 2025.
Mkutano huo ulifanyika wakati Jiji la Kigali likiandaa Mashindano ya Dunia ya Mbio za Baiskeli yaliyoanza Septemba 21 hadi 28, 2025, yakishirikisha nchi 108.





