Al Hilal SC Omdurman ya Sudan yashuka dimbani  uwanja wa Pele kumenyana na AS Kigali

Share Now

Na Christopher Karenzi

Dunia ya soka mashariki mwa Afrika inashuhudia sura mpya katika Ligi kuu ya Rwanda (Rwanda Premier League  RPL), baada ya klabu mbili kongwe kutoka Sudan, Al Hilal SC Omdurman na Al Merrikh SC, kuthibitisha ushiriki wao rasmi na Shirikisho la soka la Rwanda   FERWAFA katika ligi hiyo.

Timu ya Al Hilal SC Omdurman ina miadi na AS Kigali  jumatatu hii katika Ligi Kuu ya Rwanda (Rwanda Premier League  RPL),ikiwa ni mechi yake ya kwanza baada ya kuthibitishwa na Shirikisho la soka la Rwanda   FERWAFA.

Rais wa timu hiyo, Yasir Hassan Ibrahim, amelishukuru shirikisho la FERWAFA kwa kuwapa fursa ya kushiriki  kwenye ligi ya Rwanda, amesema .

 ‘’  Kwa niaba ya Bodi ya wakurugenz nashukuru Shirikisho la soka la FERWAFA kwa kutuunga mkono na kukubali ujio wetu wa kushriki ligi ya Rwanda. Hapa tunajisikia kama tuko nyumbani”.

 ‘’ Sisi tupo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika (CAF Champions League), na tunaamini ligi hii itatusaidia katika maandalizi yetu. Ibrahimameongeza

Wakati huo huo, timu nyingine kutoka Sudan Al Merrikh SC tayari imewasili mjini Kigali, imeanza maandalizi ya kushiriki katika Ligi Kuu ya Rwanda. Kocha mkuu Darko Novic, kocha aliyewahi kuinoa APR FC, mabingwa watetezi wa ligi hiyo msimu uliopita alikuwa na haya ya.Kocha Darco amesema                       

Ligi ya Rwanda ni ngumu sana, si jambo rahisi kucheza hapa. Hakuna tofauti  kucheza na timu ndogo au kubwa, kwa sababu kila timu inaweza kuishinda nyingine wakati wowote’’.

 Al Merrikh itaanza mechi zake kwenye mzunguko wa 8 wa ligi, baada ya kukamilisha usajili na taratibu zote za Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa).

Kwenye michuano ya  Ligi ya Klabu bingwa Afrika, Al Hilal SC kwenye Kundi C itacheza mechi zake za nyumbani mjini Kigali, itakapovaana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, MC Alger ya Algeria, na FC Saint-Éloi Lupopo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Aidha , timu ya APR FC iliibwaga  Rayon sports mabao 3-0 katika  mchuano wa ‘’ Dabi ya Milima elfu moja’’ kwenye ligi kuu ya soka iliyopigwa kwenye uwanja wa Taifa wa Amahoro mwishoni mwa juma. Kocha mkuu wa Rayon Haruna Ferouz baada ya mechi hiyo  amefanya mazungumzo  na waandishi wa habari amesema kwamba magoli matatu kwenye derby ni mengi.Amebaini kuwa upungufu kwa timu yake ulikuwa katikati kwa wachezaji wa kiungo.

Mchezaji wa kiungo mshambuliaji Abed akitafuta mbinu za kuwaponyoka viungo wa APR

Kwa jumla timu ya jeshi la Polisi inaongoza kenye jedrwari la  ligi  katika mzunguko wa saba  na alama 17, ikifuata Rayon sports na alama  12.


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *