Aigle Noir yapangwa kukwaruzana na ASAS Djibouti Télécom

Share Now

Droo ya CAF Champions League na CAF Confederation Cup yaliyofanyika nchini Tanzania, timu mbili kutoka Burundi zimejua wapinzani wao katika hatua za awali za mashindano haya makubwa barani Afrika:

Aigle Noir SC (Burundi) itakwaruzana na ASAS Djibouti Télécom (Djibouti)

Mshindi wa mechi hii atakutana na Al Ahly (Misri), mabingwa mara nyingi wa CAF Champions League!

Kocha mkuu wa Aigle Noirs  FC Jimmy Ndayizeye akizungumzia droo kati ya Aigle Noir SC (Burundi) itakayokwaruzana na ASAS Djibouti Télécom (Djibouti), amesema tofautisha timu  za zamani za Djibouti na leo.

Viongozi wa timu hizo siku wana  sajili wachezaji wa viwango vizuri. Amesema ‘’Telecom sio mbaya  nafikiri miaka  10 iliyopita timu za Burundi zilikuwa zikifunga kirahisi timu za Djibouti hata timu  ya taifa Burundi ikiifunga. Siku hizi   wanasajili wachezaji wa kigeni. Kwetu sisi ni kujiandaa vizuri  tuangalia kama tutaweza kusonga mbele kwenye hatua ya pili.

Kocha mkuu wa Aigle Noir FC Jimmy Ndayizeye

Akichambua kuhusu  mchuano kati ya mabingwa APR na Pyramids, Kocha Ndayizeye amesema Pyramids ni timu kali wakiwa ni mabingwa watetezi wa Afrika lakini APR wanaweza kujipanga vizuri wakaiondoa. Amebaini kuwa kwenye mchezo wa soka kila kitu kinawezekana.

Kocha Ndayizeye akiongea na Brightafrica.rw amesema “ Waarabu wanapokuwa ugenini wanacheza kwa kujihami  na kutafuta  sare yoyote ile.  Wanapofika kwenye uwanja wao wanafanya mashambulizi ya hapa na pale na kukuletea presha. Wakipata mabao mawili au matatu, tayari wako kwenye mazingira mazuri ya kukuondoa’’.

Aigle Noir FC Mabingwa wa Ligi kuu ya Burundi msimu 2024-2025

Kocha Ndayizeye akiongea na Brightafrica.rw amesema “ Waarabu wanapokuwa ugenini wanacheza kwa kujihami  na kutafuta  sare yoyote ile.  Wanapofika kwenye uwanja wao wanafanya mashambulizi ya hapa na pale na kukuletea presha. Wakipata mabao mawili au matatu, tayari wako kwenye mazingira mazuri ya kukuondoa’’.

Kwa upande mwingine timu ya Flambeau du Centre (Burundi) itamenyana na Mshindi wa Kombe la Ligi kutoka Libya. Flambeau du Centre FC walitwaa ubingwa wa Kombe la Rais wa Burundi 2025 wataiwakilisha Burundi mwezi ujao kwenye mashindano ya TotalEnergies CAF Confederation Cup 2024/2025.

Flambeau du Centre FC

Christopher Karenzi


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *