Timu ya soka ya APR imetawazwa  mabingwa wa kombe la Amani (FERWAFA Peace Cup)  jana jioni baada ya kuwabwaga wapinzani wao Rayon sports  mabao 2-0  katika uwanja wa taifa wa Amahoro, jijini Kigali.

Share Now

Fainali hii ya dabi ya Milima elfu moja ilikuwa ikisubiriwa na wengi mno  kujua nani bingwa wa mwaka huu.

Mshindi wa kombe la Amani nchini Rwanda hupewa tikiti ya kushiriki kinyang’anyiro cha Shirikisho la soka barani Afrika( CAF Conferations Cup).  

Moja kwa moja APR imepata tikiti tayari ya kushiriki mashindano hayo makubwa barani Afrika. APR ina miaka 8  ilikuwa haijatwaa kombe hilo la amani.

Mugisha Gilbert wambaye umupira n’ikabutura y’umweru

Mfungaji wa bao la pili Mugisha Gilbert amesema  kwamba walkuwa na hamu sana na hili kombe: ”Tumecheza dabi 3 hapa tukigawana alama baada ya kujadiliana kwa pamoja tumeamua kutumia nguvu zetu zote ili tutwae kombe hili hatimaye imewezekana tunashukuru Mungu”.

Romario Abdul Djabar Gakuba

Romario Abdul Djabari ni mchambuzi wa michezo  anaeleza kilichosababisha kushindwa kutamba kwa Rayon, amesema ”Kupata ushindi wa mabao 2 kwa sifuri dhidi ya Rayon niseme kwamba  APR walikuwa wazuri hasa kwenye kiungo ambapo walikaba sawa sawa kwa sababu Rayon nguvu  zao ziko kwenye kiungo.Ukimpa nafasi Kevin pamoja na wachezaji wa pembeni, inakuwa shida kubwa sana”.

Huku zikisalia mechi tano kabla ya ligi kutamatika, timu ya Rayon inaongoza ligi kuu ya soka ikiwa mbele ya APR kwa alama 1.

Mshindi wa ligi kuu ya soka huwakilisha Rwanda katika michuano ya mabingwa barani Afrika (Champions League).

Rayon ilitwaa kombe hili mwaka 2023 ambapo iliipokonya mpinzani wake  APR  kwa bao 1-0.  APR ikiwa na hamu ya kombe hili ililolitwaa mwaka 2018.

Aidha  mkoani Makamba nchini Burundi timu ya soka ya Aigle Noir FC imetawazwa mabingwa msimu huu wa 2024-2025, imeipokonya jeshi la Polisi Rukinzo kwa magoli 2-0 kwenye uwanja wa Nkurunziza Peace Park complexe jumamosi.

Fleuri ni mchabuzi kutoka  jijini Bujumbura, amesema  ‘’Hadi sasa imebaki mechi moja kabla ya ligi kufikia ukingoni timu ya Aigle Noir ndio mabingwa  wa Primus League Burundi mwaka huu wa michezo  2024-25’’

Nchini Burundi inabaki wiki moja ya mchezo kabla ya kutamatika kwa ligi msimu huu wa 2024-25.

Christopher Karenzi


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *