Urusi na nchi za Magharibi kubadilishana wafungwa

Share Now

Kremlin na nchi za Magharibi zimekubaliana juu ya mpango mkubwa wa kubadilishana wafungwa, ikiwa ni pamoja na kuachiliwa kwa Wamarekani kadhaa kama vile mwandishi wa habari wa Gazeti la Wall Street Journal Evan Gershkovich anayezuiliwa nchini Urusi tangu mwaka 2023, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti siku ya Alhamisi Agosti 1

Makubaliano haya, ambayo yanaonekana kuwa muhimu zaidi tangu Vita Baridi, pia yanatoa fursa ya kuachiliwa kwa aliyekuwa askari wa kikosi cha wanamaji cha Marekani Paul Whelan, kulingana na kituo cha habari cha CNN, wakati kituo cha habari cha ABC kimeripoti kwamba nchi nyingine za Magharibi zinahusika katika mpango huu wa kubadilishana wafungwa. Ikiwa mpango huu wa kubadilishana wafungwa utafanyika, itakuwa mara ya kwanza kati ya Moscow na nchi za Magharibi tangu kuachiliwa kwa mchezaji wa mpira wa kikapu wa Marekani Brittney Griner aliyezuiliwa nchini Urusi mnamo mwezi Desemba 2022 kwa kesi ya madawa ya kulevya dhidi ya mlanguzi wa silaha maarufu wa Urusi Viktor Bout, aliyekuwa akifungwa nchini Marekani.

Mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich katika mahakama ya Yekaterinburg, Julai 19, 2024. © Dmitry Chasovitin / Reuters

Kufikia sasa hakuna uthibitisho wowote kutoka kwa maafisa wa Marekani na Kremlin imekataa kutoa maoni mapema siku ya Alhamisi. Kwa sasa, uvumi umeenea. Vyanzo vya habari vya Urusi vinasema kwamba kwa mpango wa kubadilishana wafungwa, majasusi wawili wa Urusi waliokuwa walikamatwa na kuhukumiwa kifungo huko Slovenia wameachiliwa. Mume na mkewe Artem na Anna Dultsev walirejea nchini Urusi kupitia Kaliningrad kwenye pwani ya Baltic, kabla ya kuwasili Murmansk kaskazini mwa nchi. Mpango  ambao unaweza kuhusu wengine.

Kuna mazungumzo nchini Urusi juu ya mpango wa kuachiliwa wafungwa na kuondoka kwa wafungwa kutoka nchi za Magharibi zaidi ya dazeni ya wafungwa wa kisiasa, akiwemo Vladimir Kara-Murza ambaye anatumikia kifungo cha miaka 25 jela kwa kudharau jeshi la Urusi. Habari ambayo asubuhi ya leo Kremlin ilikataa kutoa maoni yoyote, lakini hilo linaweza kutokea katika saa zijazo, anabainisha Jean-Didier Revoin, mwandishi wetu huko Moscow.

RFI


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *