Rwanda ni mwenyeji wa shindano  la soka la Afrika ya mashariki na kati CECAFA Kagame cup 2026.  

Share Now

Na Christopher Karenzi

Club ya Police FC na Kiyovu Sports  za Rwanda zinaweza kuungana na APR FC pamoja na Rayon Sports kama wawakilishi wa Rwanda katika CECAFA Kagame Cup 2026, mashindano yatakayofanyika  nchini humo kuanzia Julai 18 hadi Agosti 9, 2026.  Hayo yametangazwa naFabrice Shema,Rais wa Shirikisho la kandanda nchini Rwanda Ferwafa

APR FC na Rayon Sports tayari zimependekezwa kushiriki mashindano hayo, lakini Rais wa Shirikisho la Soka la Rwanda, Fabrice Shema, amesema kuwa shirikisho hilo linafanya juhudi za kuongeza idadi ya timu zingine 2 za Rwanda , ameeeleza: “Tuko kwenye mazungumzo ya kuhakikisha kuwa timu nne za Rwanda zinashiriki  CECAFA KAGAME CUP  badala ya timu mbili,  timu hizo ni za wanaume  ni Police na Kiyovu,”.

Shema alitoa kauli hiyo wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa FERWAFA uliofanyika mjini Kigali Jumapili, Mei 31, ambapo wajumbe walipitia na kutathmini shughuli za shirikisho kwa msimu wa mwaka 2025.Iwapo mpango huo utafanikiwa, Rwanda itakuwa na uwakilishi mkubwa zaidi katika mashindano hayo ya klabu bingwa za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Fabrice Shema amesema kwamba  baadhi  ya timu vigogo wa Afrika ya Mashariki wamekubali mwaliko kuja Kigali “CECAFA ilianza kutuma mwaliko kwa timu mbalimbali. Kuna baadhi ya timu ambazo tayari zimekubali kuja kushiriki Kombe la Kagame. Miongoni mwa timu hizo ni Simba, Yanga, Vipers, Al Hilal na Al Merrikh. Timu zote hizo tayari zimethibitisha ushiriki wao, na bado zipo nyingine’’. Pia tumealika timu kutoka kanda nyingine, zikiwemo Afrika Kaskazini na Afrika Magharibi na tunafikiria kwamba timu kutoka Tunisia, Libya na hata Mali zinaweza kuja kushiriki mashindano hayo.”

Wananchama wa FERWAFA katika Mkutano Mkuu Maalum

CECAFA Kagame Cup ni moja kati ya mashindano sita ya soka ya kikanda ambayo Council for East and Central Africa Football Associations (CECAFA) imeikabidhi Rwanda kuyaandaa mwaka 2026.

Kombe la Kagame litakuwa mashindano ya kwanza kati ya hayo, yakitarajiwa kuanza Julai 18 na kumalizika Agosti 9, 2026.  Baada ya hapo, kutafanyika mashindano ya CAF African Schools Football Championship (CECAFA Qualifiers) kuanzia Julai 22 hadi 25.

Aidha, Rwanda pia itaandaa michuano ya mchujo ya ukanda wa CECAFA ya CAF Women’s Champions League CECAFA Qualifiers kuanzia Agosti 22 hadi Septemba 6.


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *