Betty Kibaara: Wanafunzi  milioni 65 barani Afrika hupewa chakula mashuleni

Share Now

Rwanda imekuwa mwenyeji wa Kongamano la Mfumo wa Chakula Barani Afrika 2024. Zaidi ya wadau 4,500 kutoka mataifa mbali mbali barani Afrika wameshiriki Kongamano hilo  kuanzia tarehe 2-6 Septemba 2024 jijini Kigali, Rwanda.

Betty Kibaara ni Mkurugenzi wa Mpango wa Chakula  katika Shirika la The Rockefeller Foundation, Ofisi ya Kanda ya Afrika, alikuwa mongoni mwa walioshiriki kongamano hili.

Betty Kibaara ni mkenya  anayeongoza uwekezaji wa Shirika hilo katika kubadilisha mifumo ya chakula  pamoja na kuongeza upatikanaji wa vyakula vya lishe kupitia programu za chakula shuleni.

Nimeanza kumuuliza  umuhimu wa kuwekeza  mashuleni  barani Afrika, kwa kuzingatia faida za lishe, elimu na kiuchumi?

Amesema kwamba chakula kwa watoto ni muhimu sana akieleza takwimu zilivo mashuleni “Wanafunzi  milioni 65 barani Afrika hupewa chakula mashuleni. Tunapozungumza hiyo idadi barani Afrika kwa wanafunzi wanaopata mlo shuleni bado hawatoshi. Amesema Mkurugenzi Betty Kibaara.

Mkurugenzi wa Shirika la The Rockefeller Foundation Betty Kibaara

Mkurugenzi Kibaara ametoa mfano jinsi alivofaidika enzi za aliyekuwa Rais wa zamani wa Kenya Hayati  Daniel Toroitich Arap Moi. Wanafuzi walikuwa wakipata maziwa  maarufu  “ Maziwa ya Nyayo’’. Amebaini kuwa watoto wapatao milioni 4 walipata maziwa kutokana na mpango wa Nyayo wakati huo nchini humo.

Uwekezaji huu ulichochea sekta ya maziwa na kuchangia ukuaji mkubwa na kuifanya Kenya kuwa inaongoza katika sekta ya maziwa. Hebu fikiria kama tungeweza kufanya vivyo hivyo kwa minyororo mingine ya thamani kama vile mtama.

Bi Kibaara amesema miaka miwili iyopita  baadhi ya serikali zinasaidia watoto kuhakikisha wanapata chakula kupitia Muungano wa Elimu Ulimwenguni ” Global School Meals coalition”. “Nchi 100 zimesaini mkataba  wa kuunga mkono pendekezo hilo ambapo  nchi 40 barani Afrika zimethibitisha kwamba zitaweka mikakati kuhakikisha kwamba watoto wanapewa vyakula shuleni. Nchi hizo ni kama Rwanda, Kenya , Uganda na Tanzania ’’.

Mkurugenzi  Kibaara  hata hivo ana hofu kwamba baadhi ya mataifa yanahitaji kutimiza ahadi lakini kupata fedha ya kutosha kwa kila mtoto kupata chakula si rahisi.

Watu mbali mbali wakitemblea Banda la bidhaa za Shirika la Rockefeller Kigali. Bidhaa hizo ni kama unga wa posho  ambao umesagwa bila kutoa pumba na vijidudu na nafaka nzima.

Kiongozi wa Shirika la The Rockefeller ameongeza kwamba lengo  hasa la Shirika hilo ni kuhakikisha kwamba wanaongea na viongozi wa serikali mbali mbali na kujadiliana ni wapi pesa zinaweza kupatikana kwa ajili ya lishe kwa wanafunzi.

Kongamano  hili kubwa  hufanyika  kila mwaka mwezi Septemba, linajikita hasa  kuhusiana na sekta ya kilimo ambapo linawaleta kwa pamoja  watu tofauti taofauti,  wajumbe kutoka serikalini, mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’s na watu binafsi ili  kujadiliana  juu ya changamoto wanazopitia barani Afrika.

Christopher Karenzi

 








Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *