May stars Continental Cycling Team, ni muhimu sana kwa wanabaiskeli Rwanda
Criterium de Kigali ni moja ya mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la kuendesha baiskeli nchini Rwanda FERWACY ambayo yako kwenye karenda ya “Rwanda Cycling Cup”.
Washiriki wa shindano kutoka vilabu mbali mbali wanaume kwa wanawake wameshiriki shindano hilo jumapili tarehe 08.09.2023jijini Kigali kupitia njia ya BK Arena – Kimironko Simba – KIE – RRA – Airtel – Stade Amahoro – BK Arena.
Upande wa wanaume mwendesha baiskeli Mugisha Moïse wa Club ya Benediction Club kutoka mjini Gisenyi ametawazwa bingwa katika shindano maarufu ‘’Criterium de Kigali” umbali wa kilomita 86 akitumia muda wa saa mbili , dakika moja na sekunde 5 (2h 1’ 5’’).

Niyonkuru Samuel wa Club ya Les Amis Sportifs, ameshikilia nafasi ya pili akiwa nyuma kwa sekunde 4.
Mukasa Nelson ni mkufunzi wa kuongeza nguvu wachezaji lakini pia ni Team manager wa Club ya May Stars inayomilikiwa na mwekezaji kutoka Eritria.

Meneja wa timu na Kocha wa kunyoosha misuli katika May stars Continental Cycling Team
Baada ya shindano hilo kumalizika Mukasa alikuwa amesema kwamba shindano hili ni muhimu kwa vijana kwa maandalizi ya mashindano ya dunia yatakayofanyika kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Rwanda mwaka 2025.
‘’ Hili shindano limetuonyesha kwamba lina wachezaji wazuri wa Rwanda wenye vipaji, huu ni mwanzo mzuri wa kujiandaa shindano la dunia mwaka 2025 kuanzia kwa watoto vijana wadogo wasichana kwa wavulana’’.
Kuhusu Timu ya wa eritrea iliyopo hapa Rwanda May stars Continental Cycling Team, amesema kwamba ni timu ambayo iko kwenye kiwango cha kushiriki mashindano ya Bara.
Amesema na hapa namnukuu ‘’ Tutajifunza mengi sana kutoka kwa waeritria kwasababu wanaongoza barani Afrika kwa kuendesha baiskeli, Ni muhimu sana kuwepo kwa timu hii ya Eritrea ambayo hutumia wachezaji wa Rwanda na Eritrea.
Mimi naishi nao, tunafanya kazi pamoja yupo kocha mkuu wa zamani wa timu ya taifa ya Eritrea.
Aidha, Kocha Mukasa amesema kwamba timu yao imeshiriki mashindano mbali mbali ikiwa ni pamoja na Estonia, France, Italy na Dubai.
Amebaini kuwa wana mpango wa kuanza kunoa watoto wadogo wanaoendesha baiskeli ili siku za usoni wawe na timu kali.
Hili shindano’Criterium de Kigali” limekuja baada ya Rais wa Shirikisho la mchezo wa kuendesha baiskeli (FERWACY) Murenzi Abdallah kujiuzulu kazi kwa hiari yake tarehe 31 Agosti 2023.
Mbali na Bwana Abdallah aliyejiuzuru, mwingine ni Nkuranga Adolphe mkurugenzi mtendaji alijiuzulu pia.

Makamu wa rais wa FERWACY, Karangwa Francois ndiye akiongoza mkutano mkuu
Naye katibu mkuu wa FERWACY Benoit Munyankindi Benoit yuko jela kutokana na kile kilichotajwa kutowajibika pamoja na kutumia vibaya madaraka aliyopewa. katibu wa kudumu Murenzi Emmanuel yeye amefukuzwa kazi.
Kulingana na taarifa ni kwamba katika mkutano mkuu uliofanyika jumapili tarehe 10 Septemba 2023, tayari Munyankindi amefutwa kazi na Shirikisho la kuendesha baiskeli FERWACY.
Aidha, Rais wa Shirikisho hilo atachukua usukani kabla ya tarehe 21 Octoba 2023.

Wanakamati wa FERWACY
Christopher Karenzi
