Gasabo Gold Refinery Ltd kuwekewa vikwazo na Marekani

Share Now

Christopher Karenzi

Marekani, kupitia Ofisi ya Kudhibiti Mali za Watu Waliowekewa Vikwazo (OFAC) iliyo chini ya Wizara yake ya Fedha, imekiwekea vikwazo kampuni ya Gasabo Gold Refinery Ltd ya Rwanda pamoja na viongozi wake.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Marekani kuidai kampuni hiyo kuhusika katika biashara na usafishaji wa dhahabu inayodaiwa kuchimbwa na kusafirishwa kinyume cha sheria kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mpaka sasa hakuna tangazo la Kampuni hiyo lilitolewa dhidi ya Marekani.

Taarifa iliyotolewa jana Alhamisi,  Wizara ya Fedha ya Marekani ilisema kuwa Gasabo Gold ni sehemu ya mtandao unaoshutumiwa kushirikiana na waasi wa M23 katika kusafirisha madini kutoka DRC kwenda Rwanda.

Katibu wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent, alisema kuwa serikali ya Marekani haitaruhusu makundi yenye silaha kunufaika na biashara haramu ya madini ambayo inaendelea kuchochea machafuko katika ukanda huo.

Kwa mujibu wa Marekani, kundi la M23 tayari lipo kwenye orodha ya makundi yaliyowekewa vikwazo na Marekani pamoja na Umoja wa Mataifa, lakini limeendelea kutumia mapato yatokanayo na biashara ya madini kufadhili shughuli zake za kijeshi.

OFAC pia inaidai Gasabo Gold kupokea na kusafisha dhahabu inayotoka kwenye migodi ya mkoa wa Kivu Kusini, kabla ya kusafirishwa kupitia Rwanda.

Aidha, Washington inasema dhahabu hiyo hutolewa katika maeneo yanayodhibitiwa na M23, kisha husafirishwa hadi wilaya ya Rusizi kabla ya kupelekwa Kigali kwa ajili ya kusafishwa katika kiwanda cha Gasabo Gold.

Kulingana na gazeti la Bwiza.com, Marekani inadai kuwa mwanzoni mwa mwaka 2026, takribani kilo 60 za dhahabu zenye thamani ya mamilioni ya dola za Marekani zilipitishwa kupitia mtandao huo.

Marekani imesema kuwa vikwazo hivyo vimewekwa kama sehemu ya kuunga mkono utekelezaji wa Makubaliano ya Washington kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), yanayolenga kuimarisha amani na kuchochea maendeleo ya uchumi katika ukanda huo.

Mbali na kampuni ya Gasabo Gold Refinery Ltd, vikwazo hivyo pia vinawahusu viongozi wa kampuni hiyo.

Marekani imesema kuwa vikwazo hivyo vimewekwa kama sehemu ya kuunga mkono utekelezaji wa Makubaliano ya Washington kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), yanayolenga kuimarisha amani na kuchochea maendeleo ya uchumi katika ukanda huo.

Mnamo tarehe 14 Desemba, Rais Tshisekedi alisafiri hadi Luanda kwa mazungumzo na mwenzake wa Angola. Hata hivyo, alielezwa kuwa suluhisho la mgogoro huo haliwezi kupatikana kwa njia ya kijeshi pekee.

Kadiri muda wa Rais Lourenço wa uenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) ulivyokuwa ukikaribia kumalizika, alianza kuandaa mpango wa kuwaleta pamoja raia wa Kongo ili wajadiliane na kutafuta suluhisho la migogoro inayowakabili, bila kumweka pembeni upande wowote.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Tshisekedi, kupitia wajumbe wake, aliijulisha Angola kwamba nafasi yake katika mchakato huo ingebaki kuwa ya kuzungumza na raia wa Kongo ambao hawakuwa tayari kwenda Kinshasa kutokana na hofu ya usalama. Mapendekezo yao yangewasilishwa kwa Serikali ya DRC ili iyafanyie kazi.

Baada ya kupokea msimamo huo, Rais João Lourenço aliamua kuiondoa Angola katika juhudi za upatanishi zilizokuwa zinalenga kuwasaidia Wakongo kutatua tofauti zao. Angola iliishutumu Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kutotekeleza makubaliano iliyokuwa imekubali awali.


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *