Club ya Al Ahly SC ya Misri yatawazwa taji la 17

Share Now

Christopher Karenzi

Club ya Al Ahly SC ya Misri, yatawazwa mabingwa wa Mashindano ya Klabu Bingwa za Afrika kwa Wanaume 2026 baada ya kuifunga timu ya Rwanda, Police VC, kwa seti tatu bila jibu (25–20, 25–21, 25–22) katika fainali iliyofanyika kwenye BK Arena, jijini Kigali mwishoni mwa juma.

Mchezaji kutoka Cuba, Masso Alvarez, alikuwa na mchango mkubwa kwa kufunga alama 13 na kuiongoza timu yake kutwaa taji lao la 17 barani Afrika na bila kupoteza hata seti moja, pamoja na kujihakikishia kufuzu kwa Mashindano ya Dunia ya Klabu za Wanaume ya FIVB.

Kocha Mmarekani anayeionoa  Al Ahly Gordon Mayforth,  alikuwa na kauri hii baada ya fainali: Nimekuwa Zimbabwe, Zambia na Morocco. Nafikiri kiwango kipo, lakini pia kunahitajika kupewa nafasi ya kujionyesha Wachezaji kutoka Algeria, Tunisia, Misri na Libya naamini kiwango kitaendelea kupanda.

Licha ya upinzani mkali kutoka kwa washambuliaji wa Police, Bettim Mateus na Elphas Makuto, pamoja na pointi tano kutoka kwa mchezaji wa kati Frank Shyaka, timu ya Rwanda ilishindwa kuhimili kasi na nguvu za Al Ahly, ambayo walitwaa seti ya kwanza kwa ushindi wa 25–20. Police walikandikwa  na Al Ahly jumla ya seti 3 kwa  bila.

Mchezaji bora wa mashindano ya mwaka huu  2026 ni Abdelrahman Elhossiny Eissa anayekipiga katika Al Ahly SC. Abdelrahman mwenye umri wa miaka 24, alifunga jumla ya pointi 60 katika mashindano hayo.

Kocha wa Police Vollyeball club, Musoni Fred ameridhika na kujivunia kutinga fainali na  kunyakua nafasi ya pili barani Afrika

Hii ni safari ya Police VC  ambapo chini ya miaka mitatu ikishiriki mashindano haya, imefikia nafasi ya pili barani Afrika, ni hatua kubwa. Mara ya mwisho kushiriki mashindano haya ilikuwa mwaka 2024,  tulimaliza katika nafasi ya sita, na sasa tumefika nafasi ya pili.

Hiki ni kiwango kinachoonyesha tunaweza kushindania ubingwa.

Kocha Paul Bitok kutoka Kenya akiwa kwenye ngazi ya kuongoza Kamati ya makocha kwenye  katika mashindano haya, ambao yupo kwenye Bodi  ya Shirikisho la Mpira wa Wavu Afrika (CAVB?, amesema kuwa alishangazwa na timu za Rwanda kwa kufika kiwango cha juu cha mchezo wa voliboli, amepongeza sana timu ya Police VC kufika kwenye hatua ya fainali ya kombe la Afrika la vilabu bingwa.

Aidha amepongeza Serikali ya Rwanda  na washirika kwa jumla kwa maandalizi na ufanisi wa mashindano haya ya 2026.

Ka musimamo Kwa timu za mataifa jirani, KPA ya Kenya ipo kwenye nafasi ya 6, Kepler ya Rwanda  ni ya 7, Nemo stars ya Uganda ya  10, APR ni ya 11, Rukinzo ya Burundi ni ya 20 huku Prisons  Volley ball mwakilishi wa  Tz ikishikilia mkia kwenye nafasi ya 24.

Timu 3 za kwanza barani Afrika zitawakilisha Rwanda kwenye kombe la dunia  mwakani.    

Tmu ya nishati REG VC ilimaliza katika nafasi ya tatu baada ya kuishinda Petrojet Sporting Club ya Misri  kwa seti 3-1 (25-21, 25-21, 13-25, 25-17).

Timu 3 zitakazowakilisha bara la Afrika katika mashindano ya dunia ya Mchezo wa Voliboli duniani  mwakani. 

Mashindano haya yalianza tarehe 22 April na kutamatika juzi jumamosi Mei Mosi 2026.

Orodha ya timu zilivoshinda mwaka huu 2026

1. Al Ahly VC (Egypt)

2. Police VC (Rwanda)

3. Rwanda Energy Group (Rwanda)

4. Petrojet (Egypt)

5. Port Autonome de Douala (Cameroon)

6. Kenya Ports Authority (Kenya)

7. Kepler VC (Rwanda)

8. Fath Union Sport (Morocco)

9. Ghana Army (Ghana)

10. Nemo Stars (Uganda)

11. APR VC (Rwanda)

12. Nigeria Customs (Nigeria)

13. Equity Bank (Kenya)

14. General Service Unit (Kenya)

15. Kalibi SC (Ghana)

16. Sport-S VC (Uganda)

17. Litto Team VC (Cameroon)

18. Cameroon Volleyball (Cameroon)

19. AS INJS (Côte d’Ivoire)

20. Rukinzo VC (Burundi)

21. Wolaitta Dicha Sports Club (Ethiopia)

22. Black Rhinos VC (Zimbabwe)

23. Atlético Clube do Mindelo (Cape Verde)

24. Prisons VC (Tanzania)


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *