Rwanda yatoa pendekezo kwa Mushikiwabo kugombea tena kiti cha Katibu mkuu wa OIF

Share Now

Na Christopher Karenzi

Serikali ya Rwanda imempendekeza tena Louise Mushikiwabo kama mgombea wa nafasi ya Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Francophonie (OIF) kwa  nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa.  Taarifa hii imethibitishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Olivier Nduhungirehe, katika mahojiano aliyoyafanya na jarida la  Ufaransa Jeune Afrique.

Wakati ikiwa imesalia miezi kumi kabla ya kufanyika Mkutano wa 20 wa Shirika la Kimataifa la Francophonie (OIF), utakaofanyika jijini Phnom Penh nchini Kambodia, Rwanda imechukua hatua mapema kumpendekeza Bi Louise Mushikiwabo ili kuwania muhula wa tatu wa kuliongoza shirika hilo.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya kimataifa, Victor Nkindi, mageuzi yaliyoanzishwa na Louise Mushikiwabo katika mihula miwili iliyopita, yameleta mchango mkubwa katika mwelekeo wa Shirika la Kimataifa la Francophonie, hasa katika sekta ya elimu na maendeleo ya mwanamke.

Amesema: ‘’Amefanikiwa kuliongoza Shirika la Francophonie kwa kuendana na mahitaji ya wakati wa sasa, hususan katika kuwawezesha wanawake. Kupitia programu mbalimbali za Jumuiya ya Francophonie, maendeleo ya wanawake yameendelea kuimarishwa duniani kote. Aidha, walimu kutoka nchi wanachama wa Francophonie, zikiwemo Cameroon na mataifa mengine, wamekuwa wakija Rwanda kufundisha lugha ya Kifaransa, hasa katika mikoa’’.

Rais Paul Kagame akipokewa na Bi Louise Mushikiwabo kwenye makao ya OIF , jijini Paris

Bi Louise Mushikiwabo alisema kuwa nchi nyingi wanachama zilimuomba kuendelea na jukumu hili na kumuahidi kumsaidia katika kugombea tena.

Nilisema kuwa mimi si kama Abdou Diouf aliyeongoza kwa mihula mitatu. Kwa kweli jambo hilo lilinifurahisha sana na kunigusa moyo kutokana na ombi la nchi zetu wanachama. Aliongeza pia kuwa atazingatia kwanza iwapo umri wa kustaafu kulingana na sheria za Rwandaunaweza kuwa kikwaz ,kwani nakaribia Louise Mushikiwabo, alizaliwa mwaka 1961. Ameongeza’’

Akizungumza kuhusu uamuzi huo, Waziri Nduhungirehe amesema  kuwa  kwa kuzingatia utendaji mzuri na wa mfano wa Katibu Mkuu ambao umetambuliwa na kuthaminiwa sana, pamoja na mashauriano  waliyoyafanya, Rwanda imechukua uamuzi wa kuwasilisha tena Louise Mushikiwabo kugombea  tena katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa OIF, utakaofanyika mwezi Novemba 2026.


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *