AFC/M23 yateka Mulema na Luke maeeneo ya Masisi!

Share Now

Na Christopher Karenzi

Muungano wa waasi wa AFC/M23 unaendelea na mashambulizi ya kijeshi dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambapo sasa umechukua udhibiti wa maeneo ya Mulema na Luke, yaliyoko katika wilaya ya Masisi, kufuatia mapigano makali kati ya pande zote mbili.

Taarifa kutoka Jimbo la Kivu Kaskazini zinathibitisha kuwa wanajeshi wa FARDC (Jeshi la Taifa), wapiganaji wa Wazalendo, pamoja na wapiganaji wa kundi la FDLR, wamelazimika kukimbia kutoka maeneo hayo, huku baadhi yao wakielekea Ngululu kwa hifadhi.

Kwa sasa, wapiganaji wa AFC/M23 wanasemekana kuelekea karibu na kijiji chaWaloa Yungu, katika mji wa wilaya ya Walikale, ambako inaaminika kuwa na mpango wa kupanua maeneo wanayoyadhibiti.

Wakati hali inazidi kuwa mbaya mashariki mwa Kongo, mapigano pia yanaendelea katika Jimbo la Kivu Kusini, hasa katika wilaya ya Shabunda, ambapo AFC/M23 inaendelea na juhudi za kuitwaa.

Haya yote yanajiri wakati ambapo mazungumzo ya amani yanaendelea huko Doha, mji mkuu wa Qatar, yakilenga kutafuta suluhisho la kina kuhusu mizozo ya muda mrefu inayolikumba eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *