Umurava yazindua SBA Connect: Jukwaa la ajira na maendeleo ya kazi kwa Michezo

Share Now

Na Christopher Karenzi

Kigali – Sekta ya michezo nchini Rwanda imepata msukumo mpya baada ya kuzinduliwa kwa SBA Connect, jukwaa jipya la ajira na maendeleo ya kazi, lililoundwa mahsusi kwa sekta ya michezo.

Hatua hii, iliyotekelezwa na SportsBiz Africa kwa ushirikiano na Umurava, inatajwa kuwa mapinduzi katika kusaidia vijana kupata ajira na kuimarisha taaluma za michezo nchini.

Mara baada ya  kutamatisha mkutano wa wa siku mbili wa SportsBiz Africa, jijini Kigali viongozi mbalimbali  kutoka mataifa tofauti, wadau wa michezo, wakufunzi…wakiwana sauti moja ya kuimarisha michezo.  

Kwa mujibu wa Vivens Uwizeyimana, kupitia teknolojia, jukwaa hili litawawezesha watafuta kazi kupata nafasi kulingana na sifa zao, huku waajiri wakipata upatikanaji wa haraka na rahisi wa vipaji. Umurava, kampuni ina uzoefu mkubwa katika sekta ya ajira na teknolojia, imewezesha jukwaa hili kwa kutoa nguvu ya kidijitali. Tayari imeorodhesha zaidi ya kampuni 400, watu 1,300 wamepata ajira kupitia mfumo wake, na nafasi za kazi zaidi ya 5,000 zimetangazwa. Aidha, imejenga hifadhi data ya zaidi ya vipaji 20,000 katika nyanja za kidijitali na biashara

Jukwaa la kwanza la vipaji vya michezo

SBA Connect ndilo jukwaa la kwanza la aina yake nchini Rwanda, likitoa nafasi ya kipekee kwa mashirika na wataalamu wa michezo kukutana. Kupitia mfumo huu, watendaji na vijana wenye vipaji wataweza kupata fursa ambazo awali zilikuwa hazijulikani au vigumu kufikiwa.

Kwa kuanzia, SBA Connect inajumuisha makundi 14 tofauti, kuanzia riadha na ukocha, hadi masuala ya teknolojia, masoko, fedha, na uendeshaji. Pia inafungua njia rasmi za kazi katika usimamizi wa matukio, mazoezi ya mwili (fitness), na vyombo vya habari. Kwa hatua hii, sekta ya michezo nchini inachukuliwa kama sehemu muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi, badala ya kubaki kwenye pembe za burudani pekee.

Kwa Rwanda yenye idadi kubwa ya vijana, SBA Connect inatoa matumaini mapya. Vijana wengi wanatafuta njia mbadala za kazi nje ya taaluma za kiasili, na michezo sasa inachukuliwa kama chaguo halali la kitaaluma.

Mbali na ajira za moja kwa moja, SBA Connect inatarajiwa kuchangia ukuaji wa sekta nyingine zinazohusiana na michezo kama utalii, vyombo vya habari, na uzalishaji. Pia litainua viwango vya taaluma katika mashindano na mashirika ya michezo nchini.

Kwa mujibu wa SportsBiz Africa, michezo siyo tu burudani bali ni injini ya maendeleo endelevu barani Afrika. Kupitia SBA Connect, Rwanda sasa imejiweka kwenye ramani kama nchi inayotumia michezo si tu kwa ushindani, bali pia kama chanzo cha ajira na maendeleo ya uchumi.

Rais wa shirikisho la mchezo wa cricket  Stephen Musaale ni miongoni mwa walioshiriki mkutano

Mwenyekiti wa Dream Team Hamim Yahya (kulia) akiwa pamoja na CEO Mankaito Pius Ballemwa kutoka Mwanza, Tanzania walishiriki Mkutano


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *