Rwanda Basketball wanawake washindwa kutamba Abidjan

Share Now

Timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya Rwanda  wanawake  ilipokea kichapo cha alama 92-45 kutoka kwa mabingwa watetezi Nigeria katika mechi ya kwanza ya Kundi D katika mashindano ya Kombe la Afrika  FIBA Women’s AfroBasket 2025,  iliyochezwa Abidjan, Côte d’Ivoire, siku ya Jumamosi, Julai 26.

Benchi la Nigeria pia lilikuwa na mchango mkubwa, likifunga alama 37 dhidi ya 13 za Rwanda, lakini kilichoiumiza Rwanda zaidi ilikuwa ni makosa yao ya kupoteza mpira mara kwa mara, yaliyosababisha Nigeria kupata alama 25.

Timu kutoka Afrika Mashariki haikuweza  kuwa tishio kwa kipindi chote cha mchezo.

Hii ilikuwa ni ushindi wa 25 mfululizo kwa D’Tigress katika mashindano haya, mfululizo ulioanza Oktoba 2015.

Elizabeth Balogun alifunga kikapu cha kwanza kwa shuti la kati, lakini Rwanda haikuonekana kutikiswa.

Ingawa katika hatua hiyo ya mchezo Rwanda ilionekana kuwa tayari kupambana, Nigeria iliendelea kuwa na nguvu zaidi uwanjani. Walicheza kwa nidhamu zaidi na kushinda kwa tofauti ya alama 47.

Bella Murekatete aliipa Rwanda uongozi wa muda mfupi wa 4-2 kabla ya Ezinne Kalu kusawazisha kwa shuti la kati na kufanya matokeo kuwa 4-4.

Mabingwa hao wa sasa walitumia mfululizo wa alama 8-0 na timu ya Afrika Mashariki haikuweza tena kuwa tishio kwa kipindi chote cha mchezo.

Murekatete alifanya mambo ya kuvutia, ikiwa ni pamoja na kuzuia kwa ustadi shuti la aliyekuwa Mchezaji Bora (MVP) Ezinne Kalu katika robo ya tatu.

Alimaliza mchezo akiwa na alama saba. Hata hivyo, tatu bora kutoka NigeriaElisabeth Balogun, Murjanatu Musa, na Victoria Macaulay walionyesha umuhimu wao kwa kuchangia jumla ya alama 43.

Benchi la Nigeria pia lilikuwa na mchango mkubwa, likifunga alama 37 dhidi ya 13 za Rwanda, lakini kilichoiumiza Rwanda zaidi ilikuwa ni makosa yao ya kupoteza mpira mara kwa mara, yaliyosababisha Nigeria kupata alama 25.

Mechi ya pili Rwanda ilichapwa na Msumbiji kwa alama 72-55ikamaliza  mechi ya mwisho kwenye kundi D, inataraji kucheza na Senegal iliyomaliza kwenye nafasi ya pili kwenye kundi C jumapili usiku  tarehe 27 Jula 2025.

Hadi kipenga cha mwisho kupulizwa, Msumbiji iliondoka na ushindi dhidi ya Rwanda kwa alama 72-55.

Rwanda itapambana na Senegal mechi  ya 3 kusaka tikiti ya Robo fainali  ¼ ya kombe la Afrika AFRO Basket 2025 nchini Cote d’Ivoire.

Christopher Karenzi


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *