APR FC yaibandua Gaadiidka FC

Share Now

Timu ya APR FC ya Rwanda yaibandua Gaadiidka FC kutoka Somalia kwa jumla ya magoli 3-1 katika michuano miwili ya  mchujo ya kusaka tikiti ya Kombe la CAF Champions League 2024. Mechi zote mbili zilifanyika katika uwanja wa Pele, jijini Kigali.

Timu ya APR FC imeanzavizuri wiki iliyopita katika mechi za  mchujo  kusaka tikiti ya Kombe la CAF Champions League 2024 kufuatia ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Gaadiidka FC. Timu zote mbili zilisajili wachezaji wenye vipaji vya kusakata gozi vizuri.

Kunako dakika ya 55 mkameroon, Apam Bemol Assongwe anayekipiga katika club ya APR FC aliandika bao la kwanza baada ya kupokea pasi  kutoka kwa Kwitonda Alain ’Bacca’.  Mechi zote mbili zilifanyika  katika uwanja wa Nyamirambo ‘’Kigali Pelé Stadium’’.

APR FC iliiendeleza mashambulizi na katika dakika ya 88 Mugisha Gilbert aliwaamusha wapenzi na mashabiki wa APR alipoweka kimyaani bao la pili bada ya kupokea  crossi ilimiminwa na beki wa kulia Nahodha, Omborenga Fitina.

Kwa jumla ya magoli 3 -1 dhidi ya timu  ya Gaadiidka FC kutoka Somalia iliyokuwa imekisuka vizuri kikosi chake mchezo wa awali wa 1-1, yalitosha kuwaaga mashindanoni.

Kocha wa APR FC mfaransa  Thierry Froger baada ya mechi alisema vijana wake wamefanya kazi ya ziada.

‘’Nafikiri jambo la muhimu, mwanzo tuliyakiwa  kuwa na ngome imara na tumeweza kuwadhibiti baadae  Baker amefanya kazi ya ziada ya kupatikana kwa bao halafu Gilbert kafunga bao. Hii ndio  faida ya wachezaji wa akiba’’.

  APR FC   itachuana na Pyramids FC ya Misri kwa hatua ya pili ya CAF Champions League kati ya tarehe 15-17 Septemba wakati wa mchezo wa marudio ni kati ya tarehe 29  Octoba 2023.

Christopher Karenzi


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *