Dr.Mujawamariya: Si lazima kutumia mrija wa plastiki wakati wa kutumia kinywaji
Wataalam wa mazingira wanasema kwamba chupa za plastiki haziozi na zinaharibu ardhi, ni kwa mantiki hiyo watu wanaozitumia baada ya kunywa maji, hawatakiwi kuzitupa hovyo hovyo wanatakiwa kuziweka mahali kunakostahili kuwekwa uchafu.
Rwanda kama mataifa mengine duniani yanaadhimisha wiki ya mazingira. Tarehe 5 Juni kila mwaka huadhimishwa duniani siku ya mazingira.
Waziri wa mazingira nchini Rwanda Dr Mujawamariya Jeanne d’Arc ameseme kwamba kutumia vifaa vya plastiki mara kadhaa vinaleta na athari mwilini. Amesema ‘’kuna vitu vinaitwa Micro plastics ni plastiki ndogo ndogo huwezi kuziona kwa jicho tunakwenda hadi kwenye damu, kuna utafiti uliofanywa mwaka jana, unaonyesha kwamba mama anayenyonyesha , mwanae anweza kunyonya hizo plastiki ndogo ndogo ambazo huwezi kuziona kwa macho yako. Inaeleweka wazi kwamba ni athari zinazomfikia mwanadamu ikiwa ni pamoja na magonjwa yasiyopona kutokana na utumiaji wa vifaa vya plastiki.
Waziri Mujawamariya aidha amesema kuna uwezekano wa kuzuia utumiaji wa vifaa vya plastiki na haituzuru wanavoishi kama kawaida.
Amesema ’’wakati wa unapotumia kinywaji, sio lazima kutumia mrija wa plastiki ukiwa na glasi na si lazima kutumia mrija wakati ukiwa na chupa’’.
Watu wengi wakati huu nchini Rwanda wameishaelewa kutosambaza hovyo hovyo vifaa ya plastiki, wengi wanatumia chupa maalum za maji ambazo zinaweza kutumika kwa muda mrefu kwa kulinda mazingira.


Viongozi mbalimbali walishiriki kikao ili kutathmini suala la mazingira
Christopher Karenzi
