Maaskari zaidi ya 500 waliostaafu wapewa vifaa vya kuwasaidia kujikimu namaisha

Share Now

Katika kituo cha Mutobo maaskari 546 kutoka makundi mbali mbali ikiwa ni pamoja na FDLR,  tarehe  23.02.2023, walipokea vifaa vya kuwasaidia kukidhi  maisha huku Rwanda ikiendelea kuwapokea wapiganaji waliostaafu kutoka Jamhuri ya kidemokraia ya Kongo na kuwarejesha katika maisha ya kawaida.

Zoezi hili lilifanyika  katika Kituo  cha Mutobo wilayani Musanze mkoani Kaskazini mwa Rwanda ambako hutolewa mafunzo ya uzalendo kabla ya kuwarejesha katika maisha ya kawaida vijijini.

Maaskari hao wanasema kwamba wamekaa miaka mingi huko wakihofia kwamba wanaporejea  nchini Rwanda wanaweza kuuwawa. Baada ya kuwasili na kupokewa walishangaa sana, wanatolea wito kwaa wenao waliobaki nje kurejea kwa hiari yao.

Viongozi wazindua shule ya ufundi Mutobo

Straton Musoni alikuwa makamu wa kwanza wa kundi la wanamgambo FDLR,  alikwenda Ujerumani mwaka 1985. Amesema kwamba tangu walipoanza kukamatwa kwa  wanasiasa wa FDLR akiwa Ujerumani, alianza kujutia na kujisikia kuwa si mwanasiasa  tena.

Amesema  ‘’Mimi ni miongoni mwa waliofungwa tulikuwa watatu ikiwa ni pamoja na aliyekuwa  Mwenyekiti wakati huo Dr. Ignace Murwanashyaka.  Tangu wakati huo sikujihisi kuwa mwanasiasa tena. Tuliwekwa gerezani, nilifungwa miaka 6  nchini Ujerumani, baadae nilitoka gerezani lakini mwenzangu Dr Murwanashyaka  alipoteza maisha ndani ya gereza’’.

1st Sergent  Uwiduhaye Marie Chantal

1st Sergent  Uwiduhaye marie Chantal maarufu Nizane Anne marie,  alikamatwa na M 23 mwezi Novemba  mwaka 2022 na kuletwa mpakani mwa DRC na kuletwa moja kwa moja Rwanda, amesema ‘’Sikujileta, nilikamatwa na M 23 kutokana na vita iliyokuwa eneo la Rutshuro, Tongo-Nyamuragir , FDLR wapo licha ya kuwa ni wachache lakini wapo. Mapambano yanaendelea sijui idadi yao niliyoiacha kama bado ipo. Sina imani kama wote bado wapo’’.

Hayo yakiarifiwaKanali mstaafu wa kundi la FDLR Joseph Gatabazi ameeleza alivokamatwa huko mashariki mwa DRC na hapa namnukuu:

‘’Nilivuka kuelekea Congo mwaka 1994, niliisha hapo takriban miaka 28 halafu nilianza kazi katika kundi la FDLR halafu CNRD. Mwaka 2019 FRDC walizingira katika mbuga ya taifa ya wanyama ya Kauzi Byega, halafu walitukamata wakatuleta Rwanda, lakini tulikuwa na woga sana tukifiriki kuwa watatuuwa’’.

Aidha akiongea na vyombo vya habari amewaasa waliobaki katika misitu ya Kongo Kurejea nchini Rwanda ili wajenge nchi yao kuliko kuhangaika huko.

Katika kituo cha Mutobo, hutolewa mafunzo ya uzalendo kabla ya kuwarejesha katika maisha ya kawaida nyumbani kwao. Baadhi yao wamerejea nchini si kwa hiari yao bali walikamatwa vitani.

Wapewa vifaa vya kuwasaidia kujiendeleza

Nyirahabineza  Valerie ni Mwenyekiti wa tume ya taifa ya kuwaaga na kurejesha katika maisha ya kawaida waliokuwa maaskari wa RDRC,  ametoa hamasa ili warejee kujenga nchi yao kutoka misitu ya Kongo. Amesema ‘’Wanaorejea ni mchanganyiko, wanaorejea kutokana na vita  huko jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, ni wale wanaokuja wakijificha jificha. Mafundisho tunayotoa hapa kwakweli ni kuwaambia watulie, mmefika kwenu, tunawaomba watusaidie kuita wenzao waliobaki wao pia warudi nchini kwasababu serikali yajiandaa kuwapokea kwa mikono miwili’’.

Waliorejea wote  kwa jumla walikuwa katika makundi mbali mbali ya wapiganaji wakiwemo wale wa FDLR.

Wamepewa vifaa vitakavyowasaidia kujiendeleza,  hupewa semina ya miezi sita. Wameelimishwa  mengi ikiwa ni pamoja na historia ya nchi, utamaduni, jinsi ya kubuni miradi, mafunzo ya uzalendo.Zoezi hilo liliongozwa na mgeni wa heshima katibu wa serikali katika wizara ya elimu anayehusika na masula ya teknolojia, shule za ufundi Irere Claudette, Kamanda wa majeshi ya nchi kavu Luteni Gen Mubaraka Muganga, ngazi za polisi na kiraia pamoja mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Rwanda akiwemo Balozi wa  Israel Ron Adams.

Kuanzia mwaka 2001 zaidi ya maaskari wa zamani  70,000  wamerejeshwa katika maisha ya kawaida  kutoka katika makundi  ya Ex FAR , Ex RDF na Ex RPA.

Musoni Straton aliyekuwa makamu wa kwanza wa FDLR

Viongozi waliohudhuria zoezi la kutoa vifaa kwa maakari wa zamani wa FDLR

Christopher Karenzi


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *