WWF – APAC: Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Afrika 2021-2025

Share Now

Kongamano kuhusu hifadhi ya mazingira jijini Kigali  iliyofanyika kuanzia tarehe 18 lilitamatika  tarehe  23 Julai 2022 iliwaleta kwa pamoja zaidi ya watu 2,500 kutoka nchi mbali mbali

Kwa wiki nzima washiriki wa mkutano walikuwa wakijadili uwakilishwaji na kuhakikisha uwepo wa wanajamii kwenye hifadhi ya mazingira haswa ukizingatia kwamba rasilimali za siri ziko kwenye jamii.

Kumezinduliwa ripoti  ambayo inazungumzia  jinsi pesa zilizotengwa  kwa minajiri ya  kuhifadhi, zinawafikia walengwa ambao ni mashirika yanayofanya uhifadhi barani Afrika

Jean Bakouma ni Mkurugenzi wa uhifadhi wa Bonde la Congo, akiwa na makao nchini Cameroon, akiongea na brightafrica.rw kuhusu kongamano hilo, amezungumzia juu ya maeneo ya uhifadhi katika bara la  Afrika, amesema ‘’Tulichukua fursa hii kujadiliana kuhusu mkakati wetu wa Afrika juu ya uhifadhi wa maeneo yaliyohifadhiwa ya Afrika.

Utazingatia mambo muhimu ambayo  ni muhimu, kuna mkakati unaohitaji mpangilio mzuri, ambao naweza kusema kwamba kuna utaratibu mzuri na utawala bora, utaratibu mwafaka na madhubuti wa kuchukua maamuzi’’.

Bakouma ameongeza kuwa  jambo jingine ni taratibu wa utekelezaji wa kujenga kwa ushirikiano na wadau ili kuhakikisha ushirikishwaji wao katika hatua zitakazopelekea kuwa na uhalali.  

 Bakouma  alisema kuhusu utelelezaji wa mpango  huo ‘’mpango mkakati mpya wa WWF Afrika unatoa mfumo wa kuunganisha kazi ya Shirika katika kanda na kupata matokeo  ili kuimarisha uhifadhi barani Afrika’’.

Hata hivyo kuna changamoto, ahadi hizi kutimizwa na mtu mmoja au shirika moja si rahisi.

Bwana Bakouma  alisema inabidi wawe na sauti moja ‘’Ni lazima tushughulikie changamoto na fursa hizi pamoja  kama nguvu zetu,  mkusanyiko  katika jamii, nchi, sekta na mitazamo ya sera inayokuja pamoja kama sauti moja.

Alice Ruhweza Mkurugenzi wa WWF Afrika

Alice Ruhweza ni mkurugenzi wa kanda ya Afrika  amefanya kazi na shirika hilo tangu julai  2019,

Ni miongoni mwa walioshiriki kongamano la hifadhi ya mazingira.

Jukumu lake ni kuendeleza na kuongoza Shirika la hifadhi  la WWF barani Afrika ili iwe na ushawishi mkubwa na kuwa na ajenda barani Afrika.

Phili Muruth makamu Mwenyekiti wa AWF

Mara baada ya kutamatika  kongamano hili, nilioongea pia na Philip Muruth, Makamu Mwenyekiti wa Shirika la uhifadhi wa mazingira na wanyama pori  African Wildlife Foundation. Nilianza kumuuliza umuhimu wa mkutano huo.

Alisema nchi 53 zilishiriki na nchi 27 zilitoka mataifa mengine duniani zilishiriki kongamano lenyewe jijini Kigali,  mkutano huo ulikuwa muhimu kwani ni mara ya kwanza kufanyika Africa parca Congres ilikuwa mara ya kwanza kukutana na kujadiliana tutahifadhi mazingira namna gani, kanini na kwa faida ya akna nani?

Miongoni mwa maazimio ya kongamano, waliazimia kuwa wanawake (Gender balance) na vijana, hao ndio viongozi wa sasa. Wamekubaliana pia kuhusu mabadiliko ya tabia nchi (Climate change)

Muruth amesema’’ Hii itatuathiri vibaya inabidi kupunguza makali juu ya mabadiliko ya tabia nchi, hizi sehemu za uhifadhi’’.

Kama mkenya alifurahia jiji la Kigali lilivopambwa na kupandwa miti sehemu  ambazo ni za  kimaumbile ndani ya mji.

Philip Muruth, amefanya katika Shirika la African Wildlife Foundation zaidi ya miaka 20.

Bara la Afrika lina takriban elfu nane na mia tano sehemu ya maeneo yaliyohifadhiwa huku takriban watu milioni miatatu wakitegemea hifadhi hizi kwa pato lao la kila siku.

Kigali city

Christopher Karenzi


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *