Mjini Kigali kunafanyika Kongamano la kimataifa  la wiki moja kuhusu  maeneo ya hifadhi barani Afrika

Share Now

Kongamano hili  limeanza tarehe 18 hadi Julai 23, 2022, limewaleta kwa pamoja watu zaidi ya elfu mbili mjini  wakiwemo  viongozi, wadau na wananchi kutoka mataifa mbali mbali wakijadili juu ya faida ya maeneo hifadhi katika kuhifadhi mazingira barani Afrika.

Nancy Githaiga ni mkurugenzi  wa shirika la African Wildlife Foundation AWF  likiwa na makao yake nchini Kenya, amesema kwamba ili kuziba pengo la maeneo ya hifadhi (protected areas), sehemu hizo ni zile  za serikali na zile za  watu binafsi  ambazo husimamiwa na jamii.

Barani Afrika wanaongelea takriban elfu 8,600 sehemu ambazo zimehifadhiwa . Miongoni mwa hifadhi hizo ni mbuga ya wanyama ya Serengeti nchini Tanzania, mbuga ya wanyama ya Nairobi na Virunga upande wa Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda.

Bi Githaiga amesema ‘’ Wanyamapori na mchanga wetu ni rasilimali yetu  waafrika hatuna maendeleo ya kiviwanda  kwa hivo hii ndio rasilimali yetu’’.

Ili kufanikisha kuziba pengo upande wa sehemu za hifadhi, mkurugenzi Githahaiga amebaini kuwa dolla  milioni 7 kwa mwaka zonahitajika kusaidia angalau kila mwaka zoezi hilo la hifadhi.

Ka upande wa Afrika ya mashariki Bi Gathaiga, ameongeza kuwa wanaafrika ya mashariki wangekuwa mbali zaidi, eti mambo muhimu wanayofanya yanabadilika.

Mkurugenzi Nancy Githaiga

Kongamano hili la kimataifa kuhusu  maeneo ya hifadhi, limeandaliwa na IUCN Africa Protected Areas Congress pamoja na African Wildlife Foundation (AWF).

Christopher Karenzi


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *