CECAFA : Toleo la mwaka huu 2026 latarajiwa kuwa na ushindani mkubwa

Share Now

Na Christopher Karenzi

Rwanda ni mwenyeji wa mshindano ya CECAFA Kagame Cup 2026, ni mashindano makubwa  ya vilabu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Yatafanyika kuanzia Julai 24 hadi Agosti 7, 2026, katika viwanja vya Amahoro Stadium na Kigali Pelé Stadium, jijini Kigali.

Kwa mujibu waShirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA) limetangaza kuwa mechi za ufunguzi za mashindano yaCECAFA Kagame Cup 2026zitachezwa katikaUwanja wa Amahoro  Ijumaa, tarehe 24 Julai 2026.

Mashindano haya yanayoshirikisha klabu kutoka Afrika Mashariki na Kati yamekuwa yakifadhiliwa na Rais Paul Kagame tangu mwaka 2002. Mara ya mwisho kufanyika nchini Rwanda ilikuwa mwaka 2019.

APR FC

Mwaka huu, mashindano yatashirikisha timu 12 zilizogawanywa katika makundi matatu. Timu zitakazoziwakilisha Rwanda ni APR FCna Rayon Sports.

Mechi za ufunguzi za CECAFA Kagame Cup 2026 zitakuwa za Kundi A, na zote zitachezwa katika Uwanja wa Amahoro siku ya Ijumaa.

Kuanzia saa 9:00 alasiri, Vipers FC ya Uganda itacheza dhidi ya Garde Républicaine FC ya Djibouti.

Mechi inayosubiriwa kwa hamu zaidi siku hiyo itaanza saa 1:00 jioni, ambapo APR FC ya Rwanda itamenyana naGor Mahia ya Kenya.

Kabla ya mashindano haya kuanza, tarehe 18 Julai 2026, kulifanyika  hafla  ya Rayon  Day, mwaka huu iliaalikwa Gormahia FC ya Kenya, mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Pele  jijini Kigali.

Wenyeji Rayon, waliibwaga Gormahia mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki.

Toleo la CECAFA mwaka huu linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ushiriki wa baadhi ya timu  zenye historia na mafanikio makubwa katika ukanda huu

Jean-Baptiste Musabyimana, Makamu Mwenyekiti wa Rayon sports, kuelekea mashindano haya ya CECAFA  alitoa kauli hii  “Tumepata nafasi nzuri kupitia mashindano haya ya CECAFA tunayokwenda kushiriki. Yakimalizika, yatatupa picha halisi ya kiwango cha timu hii. Lakini mnaijua CECAFA ilivyo. Hata hivyo, kombe liko nyumbani kwetu, na tutafanya kila liwezekanalo ili libaki hapa.”

Mwaka uliopita, 2025, Singida Black Stars ya Tanzania ilitwaa ubingwa wa mashindano ya CECAFA  baada ya kuifunga Al Hilal Omdurman ya Sudan kwa mabao 2-1 katika fainali. APR FC, iliyoiwakilisha Rwanda, ilimaliza mashindano katika nafasi ya tatu

Makundi ya CECAFA Kagame Cup 2026:

Kundi A:APR FC (Rwanda), Vipers SC (Uganda),Gor Mahia (Kenya), FC Garde Républicaine (Djibouti)

Kundi B:Singida Big Stars (Tanzania),Simba SC (Tanzania),Jamus (Sudani Kusini),Mogadishu City (Somalia)

Kundi C: Al Hilal SC (Sudani),Rayon Sports (Rwanda),Tusker FC (Kenya), KVZ SC (Zanzibar)


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *