Mashindano ya Golf ya SportsBiz Africa yarejea Kigali kwa Toleo la Pili kubwa zaidi

Share Now

Na Christophert Karenzi

chriskarenzi@gmail.com

Jukwaa la SportsBiz Africa (SBA) limetangaza kurejea kwa mashindano yake ya kimataifa ya golf, SportsBiz Africa Golf Championship, ambapo toleo la pili limepangwa kufanyika kuanzia tarehe 10 hadi 13 Septemba 2026 katika Kigali Golf Resort & Villas jijini Kigali.

Mashindano hayo, ambayo ni sehemu ya Sunshine Development Tour – East Africa Swing, yanatarajiwa kurejea kwa kiwango kikubwa zaidi, yakithibitisha nafasi ya Rwanda kama kitovu kinachochipukia cha golf ya ushindani barani Afrika.

Baada ya mafanikio ya kihistoria ya toleo la kwanza mwaka 2025, mashindano haya yanarejea huku yakivutia hamasa kubwa zaidi kimataifa na ushiriki mpana zaidi. Mwaka uliopita, tukio hilo liliwakutanisha wachezaji 105 kutoka nchi 12, wakiwemo kutoka Ulaya na Amerika, na kuweka rekodi kama mashindano ya kwanza nchini Rwanda kutoa alama za Official World Golf Ranking (OWGR) na World Amateur Golf Ranking (WAGR), hatua iliyoiweka nchi kwenye ramani ya golf duniani.

Baada ya mafanikio makubwa ya toleo la kwanza mwaka 2025, mashindano haya yanarejea yakiwa na mvuto mkubwa zaidi kimataifa. Toleo la mwaka uliopita liliwakutanisha jumla ya wachezaji 105 kutoka nchi 12, wakiwemo washiriki kutoka Ulaya na Amerika.

Kwa mara ya kwanza nchini Rwanda, mashindano hayo yalitoa alama za: Official World Golf Ranking (OWGR) , World Amateur Golf Ranking (WAGR)

Hatua hii muhimu  inaiweka Rwanda rasmi kwenye ramani ya Gofu duniani.

Toleo la 2025 lilishuhudia ushindi wa kihistoria wa mchezaji wa kulipwa wa Rwanda, Celestin Nsanzuwera. Ushindi wake wa nyumbani ulikuwa tukio la kipekee lililoashiria hatua mpya kwa mchezo wa golf nchini.

Celestin Nsanzuwera, bingwa wa shindano la kimataifa la golf 2025

Mbali na kuboresha nafasi yake katika viwango vya kimataifa, ushindi huo uliibadilisha taswira ya golf nchini Rwanda kutoka kuwa mchezo wa watu wachache hadi kuwa mchezo wa ushindani unaozidi kupata umaarufu wa kimataifa.

Aidha. toleo la mwaka 2026 linatarajiwa kuvutia zaidi ya wachezaji 150 wa kulipwa na wa ridhaa (amateur) kutoka kote barani Afrika na kwingineko duniani, hatua itakayoongeza kiwango cha ushindani na kupanua wigo wa mashindano hayo.

Mashindano hayo ya siku tatu yatachezwa kwa mfumo wa mashimo 54, yakitoa jumla ya zawadi ya dola za Marekani 25,000 (takriban shilingi milioni 36.5 za Rwanda).  Washiriki watapata fursa ya kujikusanyia alama muhimu za: Sunshine Development Tour Order of Merit , Official World Golf Ranking (OWGR) na  World Amateur Golf Ranking (WAGR) .

 Waandaaji Wasisitiza Umuhimu wa Mashindano Afrika

Akizungumza kabla ya mashindano hayo, Promota wa Sunshine Development Tour – East Africa Swing, Charles Gacheru, alieleza kuwa tukio hilo linaendelea kuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha mfumo wa ushindani wa mchezo wa golf barani Afrika, Amesema:

“Mafanikio ya toleo la kwanza lililofanyika Kigali yalionyesha wazi uwezo mkubwa uliopo katika ukanda huu, si tu kwa upande wa vipaji bali pia uwezo wa kuandaa mashindano ya kiwango cha kimataifa. Mwaka huu, tunaendeleza mafanikio hayo kwa kupanua ushiriki na kuunda fursa zaidi za ushindani kwa wachezaji kujipatia alama za viwango na kupiga hatua katika mfumo wa kimataifa wa golf,” amesema.

Athari Chanya kwa Maendeleo ya Michezo Rwanda

Kwa upande wake, Kiongozi wa  Jukwaa  la SportsBiz Africa, Christian Gakwaya, amesisitiza mchango wa mashindano hayo kwa maendeleo ya michezo nchini Rwanda na kwa ujumla. Amesema : “Mashindano haya ni zaidi ya tukio la michezo; ni sehemu ya dira ya SBA ya kujenga rasilimali za michezo zenye hadhi ya kimataifa, zinazounganisha michezo na biashara huku zikichochea maendeleo endelevu.

Aidha ameongeza  ujumbe wa ubora wa michezo hii: ‘’ Tunapoendeleza tukio hili kuwa jukwaa la kudumu na la kiwango cha juu, hatuionyeshi tu Rwanda kama kituo bora cha michezo ya kimataifa, bali pia tunaunda fursa zenye tija kwa vipaji vya ndani, wadau, na mfumo mzima wa michezo,” ameeleza.

Rwanda Yaendelea Kujiimarisha Kama Kituo cha Michezo ya Kimataifa

Kadri Rwanda inavyoendelea kujipanga kuwa moja ya vituo vinavyoongoza kwa kuandaa matukio ya michezo ya kimataifa, kurejea kwa SportsBiz Africa Golf Championship kunaashiria kasi endelevu katika maendeleo ya mchezo wa golf. Aidha, kunaimarisha njia kwa wachezaji wa Afrika kushiriki na kushindana katika majukwaa ya kimataifa.


🏌️ Kuhusu Sunshine Development Tour – East Africa Swing

Sunshine Development Tour – East Africa Swing ni mzunguko wa mashindano ya kitaaluma ya golf unaolenga kuwapa wachezaji bora wa Afrika — wanaume na wanawake — fursa za kushiriki mashindano yenye ushindani wa hali ya juu. Mashindano haya yanaendeshwa kwa ushirikiano na Sunshine Tour.

Msimu wa mwaka 2026 unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi, ukiwa na jumla ya mashindano 14 katika ukanda wa Afrika Mashariki. Aidha, kutaanzishwa mzunguko mpya wa Afrika Magharibi kupitia mashindano ya Alpha Bravo Golf Classic yatakayofanyika Lagos, Nigeria.

 Kuhusu Jukwaa la SportsBiz Africa

SportsBiz Africa Forum ni tukio la kila mwaka linalolenga kukuza mchango wa michezo kama chombo cha maendeleo endelevu barani Afrika.

Likiongozwa na dira ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika, SportsBiz Africa inaona michezo kama nyenzo muhimu ya: kuimarisha umoja na mshikamano  kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi

Mashindano ya SBA Golf Championship ni moja ya matukio makuu yanayoandaliwa sambamba na jukwaa hilo. Matukio mengine ni pamoja na: Mkutano wa Watunga Sera (Policymakers Roundtable),  Jukwaa la Wawekezaji (Investors Dealroom), Mashindano ya SBA Esports Cup na Programu ya Mafunzo Mtandaoni kwa Vijana wa Afrika.

Celestin Nsanzuwera, bingwa wa shindano la kimataifa la golf 2025


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *