Watu 13 wapoteza  maisha nchini Burundi kutokana na milipuko ya moto

Share Now

Jeshi la Burundi limesema kuwa milipuko iliyotokea katika ghala la kuhifadhi risasi nchini humo, imewaua watu 13 na kuwajeruhi wengine 57.

Taarifa hizo zimetolewa na Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Burundi, Brigedia Jenerali Gaspard Baratuza, alipozungumza na vyombo vya habari. Kulingana na Baratuza, milipuko hiyo ilitokea katika eneo la Musaga, Manispaa ya Muha, jijini Bujumbura.

“Milipuko iliyosababishwa na moto huu ilisababisha uharibifu mkubwa, wa mali na binadamu. Watu 13 walikufa na wengine 57 walijeruhiwa, yaani raia 54 na wanajeshi 3.

Kulingana na DW, Nyumba ziliharibiwa katika mitaa mbalimbali, pamoja na magari ya watu binafsi. Vifaa na miundombinu ya kijeshi pia viliteketea au kuharibiwa,”alisema Brigedia Baratuza.

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye alitoa pia salamu za rambirambi kwa walioathirika na mkasa huo

Jeshi limewahakikishia wananchi wa Burundi kuwa licha ya hasara iliyopatikana, usalama nchini humo umesalia kuwa imara.

Habari zaidi zinaeleza kuwa Moto huo pia ulisababisha kukatika kwa umeme katika kambi hiyo inayofahamika kama “Base” na vitongoji vyake, ambapo wakazi wa maeneo ya Gasekebuye, Kanyosha, Kinindo na kwengineko walitakiwa kutokuwa na hofu. Hali ya utulivu imerejeamjini Bujumbura  baada ya taharuki kufuatia milipuko hiyo huku mamlaka zikieleza kuwa watoto waliokimbia wakiwa peke yao wakati wa tukio hilo sasa wapo katika Parokia ya Kanisa Katoliki ya Buhonga wakisubiri kukutanishwa tena na familia zao.

Christopher Karenzi


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *