Benin yatangaza kikosi cha wachezaji 25 kwa michezo ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Rwanda

Share Now

Na Mwandishi Christopher Karenzi

Timu ya Taifa ya Benin imetangaza kikosi cha wachezaji 25 kitakachoshiriki katika michezo miwili muhimu ya kufuzu Kombe la Dunia la 2026, ikiwemo mechi dhidi ya Rwanda (Amavubi) itakayochezwa jijini Kigali, na ile dhidi ya Nigeria.

Kikosi hicho kimetangazwa na kocha mkuu Gernot Rohr usiku wa Ijumaa, tarehe 3 Oktoba 2025, ikiwa imebaki wiki moja kabla ya michezo hiyo muhimu kuchezwa.

Orodha ya wachezaji walioitwa

Makipa: Saturnin Allagbé, Marcel Dandjinou, Serge Obassa


Walinzi: Olivier Verdon, Mohamed Tijani, Yohan Roche, Tamimou Ouorou, Cédric Hountondji, David Kiki, Rodrigue Fassinou


Viungo: Dodo Dokou, Mariano Ahouangbo, Mattéo Ahlinvi, Imourane Hassane, Samadou Attidjiko, Sessi D’Almeida, Rodrigue Kossi


Washambuliaji: Steve Mounié, Jodel Dossou, Tosin Aiyegun, Junior Olaitan, Romaric Amoussou, Razack Rachidou, Andreas Hountondji, Olatoundji Tessilimi

Timu ya taifa ya Benin

Benin itaanza kampeni yake kwa kucheza ugenini dhidi ya Rwanda tarehe 10 Oktoba 2025 kwenye Uwanja wa Amahoro, katika mchezo unaotarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa kwa pande zote mbili zinazowania nafasi ya kufuzu. Kwa upande wa Amavubi, ushindi utakuwa muhimu ili kupanda kwenye msimamo wa Kundi C, ambapo kwa sasa wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi 11. Benin, kwa upande mwingine, inaongoza kundi hilo kwa pointi 14 na inalenga kuendeleza ubabe wake.

Baada ya mchezo dhidi ya Rwanda, Benin itacheza mechi yake ya pili dhidi ya Nigeria tarehe 14 Oktoba 2025, mchezo mwingine wa kuamua mustakabali wa mbio za kufuzu kwa Kombe la Dunia litakalofanyika Marekani, Mexico na Canada.

Hali ya msimamo wa Kundi C (kabla ya michezo ijayo)

NafasiTimuMechiPointi
1Benin714
2South Africa716
3Nigeria711
4Rwanda711
5Lesotho77
6Zimbabwe74

Benin ina matumaini ya kuendeleza rekodi nzuri baada ya kuonyesha ubora katika michezo ya awali, huku Amavubi wa Rwanda wakitarajia kutumia faida ya kucheza nyumbani ili kupata ushindi muhimu mbele ya mashabiki wao.

Tukiwa kwenye ukanda wa maziwa makuu, Timu ya taifa ya soka ya  Burundi ‘’Intamba mu Rugamba’’, matumaini ya kufuzu fainali za  kombe la dunia  mwaka 2026, tayari yamefifia hata wakifunga mechi 2 zijazo.

Timu ya taifa ya Intamba mu Rugamba

Kulingana na Mchambuzi wa habari za Michezo nchini Burundi Nkundirinfura  Fleury, kwenye mkutano na waandishi wa habari ijumaa tarehe 03 Octoba 2025,  Kocha mkuu wa timu ya Burundi ‘Intamba ‘Mu Rugamba Sangwa Patrick, alifahamisha vyombo vya habari kwamba kuwa  lengo ni kusaka tikiti ya kushiriki fainali za Kombe la mataifa AFCON mwaka 2027  kama alivosasaini mkataba wa kuinoa timu ya  Burundi angalau kuwa pamoja na timu hiyo kwa muda wa miaka 3, timu itakuwa imara.

La msingi kwa Timu ya  ya Taifa ya Burundi ni kuwafunga Harambe stars ya Kenya kwenye uwanja wa kisasa wa ‘’Intwari’’ jijini Bujumbura alhamisi tarehe 09 Octoba 2025. 


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *