Handball: NCPB Kenya yatawazwa mabingwa ‘ECAHF Senior Club Championship’ 2024
Timu ya Handball ya wanaume ya Bodi ya kitaifa ya Nafaka na mazao kutoka nchini Kenya (NCPB) mabingwa watetezi wa ukanda wa Afrika ya mashariki mwaka jana, wameendeleza ubabe jumamosi tarehe 21 octoba 2024.
Wametawazwa mabingwa wa Ukanda wa Afrika ya Mashariki baada ya kuwachapa Polisi ya Rwanda kwa magoli 30-27 katika uwanja mdogo wa Amahoro jijini Kigali.

Upande wa wanawake Police WHC ya Uganda ilitawazwa mabingwa wa ukanda huu kufuatia ushindi mnono wa magoli 61-27 dhidi ya Chuo kikuu cha Kigali. Upande wa wanaume kuwania nafasi ya 3, jumamosi tarehe 21 Disemba 2024, APR HC iliilaza S.O.S ya Burundi kwa magoli 36-29 wakati timu ya wanawake ya Nairobi Water kutoka Kenya ikiwachapa ESC Nyamasheke ya Rwanda ikiichapa 28-21.
Katika kuwania taji la ubingwa wa Afrika ya mashariki (ECAHF) mwaka huu iliyofanyika jijini Kigali, Rwanda, kocha mku wa timu ya Rwanda National Police Antoine Ntabanganyimana akiongea na brightafrica.rw amesema kwamba kipindi cha kwanza walicheza vizuri lakini katika kipindi cha pili, walipunguzwa kasi ya mchezo.

Coach Antoine Ntabanganyimana wa RNP HC
Alikuwa na haya ya kueleza ‘’ katika kipindi cha pili Kwa bahati mbaya Wapinzani walisawazisha tukaenda kwenye dakika za nyongeza (Extra time) tukafungwa’’.
Kocha Antoine Ntabanganyimana amebaini kuwa vijana wake walikuwa na uchovu ‘’ Jana tulicheza mechi kali dhidi ya APR, leo wamechoka lakini tusisingizie uchuvu tulijaribu ni kwa bahati mbaya tu tulifungwa ’’.
Kocha mkuu wa National Cereals and Produce Board (NCPB) Kenya, Bryan Mathews akiongea na Bightafrica.rw ameeleza furaha yake baada ya kupata ushindi ambapo haikuwa rahisi. Amesema Polisi ni timu nzuri ila mnamo kipindi cha pili walilegeza.

Kocha Mkuu wa NCPB Kenya Byran Mathews akia pamoja na mchezaji wake
Katika kipindi cha mapumziko Rwanda National Police Handball (RNP) ilikuwa ikiongoza kwa tofauti ya magoli 6. Byran amelezea siri ya ushindi ‘’ Niliwaambia vijana wangu kuwa Kikombe ni chetu hakuna mechi nyingine baada ya hiyo, tuna safari ndefu kurudi nyumbani na itakuwa huzuni kurudi nyuma kwa muda wa siku mbili kwa njia ya barabara’’.
Vijana walifikiria hilo wakajitahidi kurejea uwanjani wakiwa wamebadili mtindo wa mchezo na morali ya hali ya juu ambapo kila mmoja alisukuma mwenzake na mlindamlango alikuwa imara kuzuia hatari langoni hatimaye wakaondoka na ushindi.
Aidha, NCPB na mwenzake wa Rwanda Polisi zilizocheza fainali zimefuzu kushiriki fainali ya Kombe la Afrika kwa timu za vilabu bingwa mwakani 2025.
Timu zilizoshiriki shindano hili ni kutoka Uganda, Kenya, Sudan Kusini, Burundi na Mwenyeji Rwanda.





Christopher Karenzi
