Nchini Rwanda zipo timu 3 bora ambapo kila mmoja inapambana ili iweze kushiriki mashindano ya kimataifa ya mpira wa kikapu Basketball Africa League (BAL) .

Share Now

Timu ya APR BBC ni mwakilishi wa Rwanda katika fainali za kombe la BAL, imefanya usajiri huku ikijiandaa mashindano ya mchujo ya BAL.  Jumatano wiki hii  ilipata chamtemakuni, ilifungwa  na Patriots BBC kwa alama 73-59  ni dabi ya Kigali.

Kocha mkuu wa Patriots  mtanzania Henry Mwinuka alifanya mahojiano na RFI Kiswahili-michezo. Aidha, aliifunga timu ya nishati  REG  wiki iliyopita na wiki hii  amichapa APR.  Kocha Mwinuka  ametwaa vikombe 5 vya ligi katika timu mbili tofauti REG na Patriots katika uwanja wa LDK . Amesema asilimia 80 anatwaa ubingwa wa ligi msimu huu.

Hakuna kocha mwingine hapa nchini ambaye amethubutu kufanya kitendo kama hicho kwa timu mbili kabambe. 

APR iko kwenye kundi moja na US Monastir mabingwa watetezi wa BAL 2022, AS Duanes yaSenegal pamoja na River Hoops ya Nigeria kuanza tarehe 4-12 Mei 2024.at STECOL.

Mechi hii ya kirafiki itasaidia APR kujiandaa mashindano ya mchujo kuelekea  mechi za  hatua ya Robo fainali ya Kombe la BAL.

Hayo yakiarifiwa, timu ya FUS Rabat  kutoka Moroc na Petro de Luanda  ya Angola tayari zimefuzu fainali  kushiriki mashindano ya BAL jijini Kigali mei baada ya kushinda mechi zao nchini Afrika ya Kusini mwishoni mwa juma. 

Timu hizo zilikuwa pamoja na  Dynamo kutoka nchini  Burundi lakini ilifurushwa kabla ya kucheza mechi yake ya pili wakiwa  nchini Afrika ya Kusini. Kisa na mkasa walikataa kuvaa jezi zenye maandishi  ya visit Rwanda.

Shirikisho la mpira wa kikapu  nchini Burundi  liliwakataza wasivae hizo jezi  ambapo mdhamini mkuu ni Rwanda kupitia mradi wa Visit Rwanda.

Hii imepelekea kusimamishwa kwa timu hiyo  kwa kipindi cha miaka mitano na kutozwa faini ya dola za kimarekani laki tano.

Christopher Karenzi


Share Now

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *